SALUFU:VIONGOZI WASIOWAJIBIKA CCM WATUPISHE

Na Francis Godwin,Darmpya Iringa

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa chama cha mapinduzi ( CCM) wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Yohanes Salufu amewataka viongozi wa vitongoji na vijiji wa CCM ambao wanashindwa kutekeleza majukumu yao kujitathimini na kuachia nafasi hizo.

Ameyasema hayo, leo wakati wa kikao cha viongozi wa CCM juu ya ufuatiliaji wa ilani ya CCM katika kata ya Nyalumbu, ambapo amesema CCM imejipanga kuona inaendelea kuchukua dola na haiwezekani kama viongozi wa CCM ngazi za chini wakawa kikwazo kwa wananchi na chama.

Aidha amesema, lazima viongozi hao kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi na kuona kata ya Nyalumbu inayoongozwa na Diwani wa Chadema inarejeshwa CCM katika uchaguzi ujao.

“Kwa kuanza lazima viongozi wa CCM kata ya Nyalumbu kuanza mchakato wa kushinda uchaguzi wa Serekali za mitaa mwakani, kazi inayofanywa na Serekali ya CCM chini ya Rais Dkt John Magufuli ni wazi mwisho wa upinzani nchini umefika mwisho ” Amesema Salufu.

Hata hivyo, ametaka viongozi wa CCM kuendelea kuwavuta wapinzani ambao hawajarudi CCM kuwahamasisha kurudi CCM, huku akisema ni aibu kwa kata ya Nyalumbu kuona vyoo vya shule vinajengwa na wafadhili huku kazi hiyo ingefaa kufanywa na wananchi .

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.