SAKATA LA MAKATO YA WASTAAFU ,SERIKALI YAIBUKA NA KUTOA NENO.

 

Na Karoli, Vinsent.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama amesema serikali imeshapata barua kutoka kwa chama cha Wafanyakazi nchini (TUCTA) inahuyosu malalamiko kuhusu ukokotoaji mpya wa mafao ya kustaafu kupitia mifuko ya hifadhi Jamii.

Waziri Mhagama ameyasema hayo jana Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa amefanya ziara kwenye ofisi ya Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (Osha).

Amesema teyari serikali imeshapata Barua kutoka TUCTA na kufikia uamuzi wa kukutana na chama hicho kwa ajili ya majadiliano na baadae kutoa kauli moja.

Waziri Mhagama amesema sheria zinazohusu masuala ya kazi na vyama vya wafanyakazi zinaitaka serikali na vyama vya wafanyakazi kukutana kwa ajili ya mashauriano wakati wowote au hata kunapotokea wafanyakazi hawariziki na jambo.

Waziri Mhagama amesisitiza kuwa lazima wafanyakazi na wananchi kwa ujumla kuangalia sheria za kimataifa zinazuhusu mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na mifumo ya mifuko ya hifadhi ya jamii yenyewe na wasiishie kulalamika tu.

Hata hivyo,Waziri Mhagama ,ameitaka OSHA kuhakikisha wanasimamia usalama kwenye ofisi za umma kuangalia mazingira kazi kwenye taasisi hizo kama ni rafiki.

Waziri Mhagama pia amewaomba waajiri nchini kujitokeza kujisajili ndani ya OSHA kutokana na kuondolewa tozo za awali ambazo zilikuwa kikwazo kwao.

Kwa Upande Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa OSHA,Khadija Mwenda ,amesema wataendelea kusimamia usalama wa wafanyakazi wote pahala pa kazi kwa kufuata kanuni na sheria zilizopo.

Mwenda amesema kwa sasa wanatoa madarasa kwa wafanyakazi nchi ili waweze kuzijua haki zao wakiwapo kazini.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.