RONALDO JUVENTUS KUMENOGA

Na Shabani Rapwi.

Mshambuliaji wa klabu ya Juventus, Cristiano Ronaldo amezidi kuwa tishia ndani ya Juventus baada ya usiku wa jana kutupia goli moja katika ushindi wa 3-0 iliyopata timu yake ya Juventus dhidi ya Sassuola, Sami Khedira ndiyo alikuwa wa kwanza kufunga goli dakika ya 23′, huku dakika ya 70′ Ronaldo akapachika goli la pili na Emre Can dakika ya 86′ akapachika goli la tatu.

Ronaldo anakuwa kinara wa ufungaji wa magoli katika Ligi Kuu ya Italia akiwa na magoli 18 akifuatiwa na Fabio Quagliarella katika nafasi ya pili akiwa na magoli 16.

Katika msimu huu kwenye mashindano yote Ronaldo ameshacheza mechi 31 na kufanikiwa kufunga magoli 20 na akitoa pasi ya mwisho (Assists) 10.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.