RC MAKONDA ATEMBELEA STAND YA MABASI MSAVU MOROGORO.

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akiwa ameambatana na Mstahiki Meya wa jiji, Mamea wa Halmashauri na Madiwani wamefanya ziara Mkoani Morogoro kwenye kituo kipya cha Mabasi  Msamvu kujifunza namna kituo hiko cha mabasi kimefanikiwa kuweka mazingira jumuishi kwa makundi yote wakiwemo wafanyabiashara na wasafiri.

Mkuu wa mkoa Makonda amesema Dar es salaam ipo katika hatua ya ujenzi wa kituo kipya cha Mabasi cha kisasa Mbezi Luis itakayogharimu zaidi ya shilingi Bilioni 50.9 ambayo itakuwa na ukubwa mara nne ya kituo cha Msamvu ambapo kitakuwa na uwezo wa kupokea Mabasi 500 kwa wakati mmoja.

Aidha Mhe. Makonda amesema kituo hiko cha Mbezi Luis kitakuwa na Jengo la Abiria,Utawala, maegesho ya mabasi, shopping mall, Hotel,Taxi, Bajaji, Pikipiki, Bank, Petrol station, Apartment, ofisi za mabasi, sehemu ya wafanyabiashara, mama Lishe,Vyoo,kituo cha polisi na sehemu ya kuhifadhi mizigo.

Pamoja na hayo Mkuu wa Mkoa Makonda ameonyesha kufurahishwa na namna kituo cha Mabasi cha Msavu kilivyoweza kuweka utaratibu mzuri kiasi cha kuongeza mapato kutoka shilingi 350,000 hadi kufikia Shilingi Million 4.5 kwa Siku.

Kwa upande wa viongozi wa Mkoa wa Morogoro wameshukuru kupokea ugeni huo mzito na wamesema watafika Dar es salaam kujifunza mambo mengi ambayo Jiji hilo limepiga hatua na kupata sifa kubwa ndani na nje ya nchi.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.