RC CHALAMILA ATOLEA UFAFANUZI KAULI YAKE ILIYOPOTOSHWA NA BAADHI VYOMBO VYA HABARI.

 

Na,Rashid Msita, Mbeya.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila atolea ufafanuzi kauli yake iliyopotoshwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini juu ya kile alichozungumza kuwa anashauri Rais aongezewe madaraka kwa kuteua watendaji wa wilaya kama ilivyokuwa kwa wakuu wa mikoa,wilaya wakurugenzi.

Mhe. Chalamila amesema kuwa habari hiyo imepotoshwa na alichozungumza yeye ni kuwa suala la msingi ni kwamba wakuu wa Idara za Halmashauri zote nchini wapatikane katika mfumo tunaopatikana watendaji wengine kama sisi.

“Yaan kwa sasa ili uwe mkuu wa Idara lazima Baraza la Madiwani likithibitishe imetokea sehemu nyingi Tanzania, Baraza la madiwani linawezakuadhimia kumfukuza au kutomthibitisha kabisa
mtumishi mwenye sifa ya kuwa mkuu wa Idara
wengi wanaothibitishwa kuwa wakuu wa Idara huanza kukaimu nafasi hizo ndipo baadae mchakato unaofuata ni kumthibitisha kuwa mkuu wa Idara ” amesema

Aidha ameongeza, inapotokea kaimu huyo akawa makini hatoi rushwa, mchapakazi,huyu hawezi kupendwa na wengi ila mabaraza mengi ya Madiwani yangempenda sana mtu anaewapa chochote na kuruhusu mengi Kwa maslahi yao.

Hata hivyo, amesema kwa mtazamo huo nikashauri sheria hiyo itenguliwe ili wakuu wa idara wapatikane katika mfumo wa kitaalamu na Madiwani wabaki kama mamlaka ya nidhamu na sio mamlaka ya mwisho ya kumthibitisha au laa mkuu wa Idara (Political works and technocratic works) haziwezii ungana wakati wote, Kuna mahali lazima
ziachane.

Ni kwa baadhi ya mabaraza ya madiwani nchini, ambpo amedai kwa upande wa mkoa wa Mbeya hilo hajawahi kujiona likitokea na likitokea lazima atashauri kwa hoja ili tija ya kiongozi iwe kwa taifa na si kwa familia.

Related posts

One Thought to “RC CHALAMILA ATOLEA UFAFANUZI KAULI YAKE ILIYOPOTOSHWA NA BAADHI VYOMBO VYA HABARI.”

  1. Pasta

    Nchi Kama tanzani swala Kama hili la uteoaji niwala ambalo halivumiliki hivyo nilazima sote tulichukulie hili swala uzito mkubwa

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.