RANGI NYEKUNDU YATAWALA LONDON KASKAZINI

Jana ligi kuu soka nchini ya Uingereza iliendea kwa michezo mitatu ambayo yote ilikuwa michezo inayozikutanisha vilabu vinavyotokea jiji moja , mapema kulikuwa na mchezo wa mahasimu wa London Magharibi Chelsea dhidi ya Fulham mchezo uliomalizika wa Chelsea kushinda 2-0, baadae kulikuwa na mchezo wa mahasimu wa London Kaskazini kati ya Klabu ya Arsenal dhidi ya Tottenham , na Arsenal kupata alama 3 kwa ushindi wa 4-2,Liverpool pia wakapata ushindi dhidi ya klabu ya Everton.
Macho ya mashabiki wengi yalikuwa upande mwa kaskazini mwa jiji london ambako Arsenal waliwalika Tottenham pale Emirates , ni moja kati michezo mizuri ndani  msimu huu wa ligi kuu soka nchini Uingereza haswa asili ya matokeo ambayo utokeaga kipind hawa imahasimu wanapokutana ,matokeo ya kuvutia uwaga zanazalishwa kwenye mchezo wa hii Derby ya Kaskazini mwa London .
Jana Arsenal walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wao Pierre Ereck Aubameyang , na baadae Tottenham wakasawazisha kupita kwa kiungo wao Eric Dier kabla ya Harry Kane kuwandikia goli la pili Tottenham  kwa mkwaju wa penati, baadae Arsenal wakazawashiza kupitia kwa Pierre kabla ya Alexander Laccazete ajapiga msumali wa 4, na kabla mwamuzi ajapiga filimbi  kiungo wa Arsenal Lucas Torreira ajapiga msumali wa 4 ma mwisho ,mpaka dakika ya mwisho Arsenal wakapata ushindi wa  4-2 (Great Derby )
Matokeo hayo yanaifanya Arsenal kurejea kwenye nafasi 4 za juu kwenye msimamo wa ligi kuu soka nchini Uingereza wakiwa na alama 30 sawa na Tottenham ila uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa yanaifanya  Arsenali kuwa nafasi ya 4 na Tottenham nafasi 5.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.