RAIS MAGUFULI AWA MGENI RASMI MISA YAKUSIMIKWA JACKSON SOSTHENES KUWA ASKOFU

Rais John Magufuli awa mgeni rasmi katika misa ya kusimikwa Jackson Sosthenes kuwa askofu wa tano wa Kanisa Anglikana Tanzania, Dayosisi ya Dar es Salaam.

Misa ya kumsimika Askofu mteule Sosthenes inafanyika asubuhi ya leo Februari 4,2018 ikiongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania, Jacob Chimeledya.

Viongozi kadhaa wa Serikali akiwemo Rais Magufuli na mkewe Janeth; Rais mstaafu Benjamin Mkapa, wanasiasa na waumini wa kanisa hilo waliwasili katika Kanisa la Mtakatifu Albano lililoko eneo la Posta jijini Dar es Salaam inakofanyika misa hiyo.

Baadhi ya viongozi waliopo kanisani ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo; Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba; Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi; Kamishna wa Uhamiaji, Dk Anna Makakala; na Waziri Ofisi ya Rais (Utumishi wa Umma na Utawala Bora), George Mkuchika.

Sosthenes anasimikwa kuwa askofu kujaza nafasi iliyoachwawazi na Dk Valentino Mokiwa aliyeondolewa madarakani na uongozi wa juu wa kanisa hilo takriban mwaka mmoja uliopita.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.