RAIS MAGUFULI AIPONGEZA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE (JKCI) KWA MAFANIKIO YAKE MAKUBWA.

Dar es Salaam. Rais Magufuli ameipongeza Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa mafanikio yake makubwa katika kutoa huduma za matibabu ya moyo hapa nchini.

Rais Magufuli ameyasema hayo mapema siku ya leo Jumatano April 18, 2018, alipotembelea taasisi hiyo kwa lengo la kuwajulia hali wagonjwa wanaopatiwa matibabu kwenye taasisi hiyo, akiwemo waziri mstaafu, Dkt. Juma Ngasongwa.

Kauli ya rais Magufuli ameitoa mbele ya mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo, Prof. Mohamed Janabi, ambapo amewamwagia sifa kedekede madaktari na wauguzi wote wa taasisi hiyo.

“Prof. Janabi, madaktari wote na wauguzi wa taasisi hii nawapongeza sana kwa kazi nzuri mnayoifanya, natambua kuwa wapo baadhi ya waliokuwa wananufaika na wagonjwa kupelekwa nje ya nchi hawatafurahia kazi mnayoifanya, lakini nyinyi chapeni kazina serikali ipo na nyinyi”, amesema rais Magufuli.

Katika ziara hiyo rais Magufuli aliambatana na mkewe mama Janeth Magufuli, ambapo kabla ya kutembelea taasisi hiyo wamepata wasaa wakwenda maeneo ya Kariakoo, nyumbani kwa wazazi wa mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, kwaajili ya kumpa pole kufuatia kifo cha mama yake mpendwa, Bi. Rehema Paulo Mombuli, aliyefariki April 13 mwaka huu, nchini India alikokuwa akipata matibabu.

Taarifa kutoka Ikulu kwa maelezo zaidi.

 

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.