RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA MUHIMBILI

 

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa 

Mheshimiwa John Pombe Magufuli amefanha ziara katkka hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kuwajulia hali wagonjwa waliolazwa katika wodi ya Mwaisela na kuwashukuru wauguzi na madaktari kwa juhudi wanazozifanya kunusuru maisha ya watu. Katika ziara hiyo mheshimiwa Rais Magufuli ameambatana na mke wake mama Janeth Magufuli wakitokea katika kanisa la Katoliki la Mtakatifu Petro lililopo oysterbay jijini Dar es Salaam ambako alihudhuria ibada ya Jumapili. Miongoni mwa wagonjwa waliojuliwa hali na rais Magufuli na mkewe ni mzee Francis Maige Kanyasu(Ngosha) ambaye alipelekwa hospitalini hapo wiki iliyopita baada ya kituo cha runinga cha Itv kutangaza habari za kuugua kwake. Rais Magufuli amewaahidi madaktari na wauguzi wa hospitali ya taifa ya Muhimbili kuwa serikali itaendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili. Kwa upande wake mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya taifa ya Muhimbili prof Lawrence Museru amemshukuru rais na kuahidi kufanya kazi kwa bidii

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.