RAIS KAGAME AMTEUA WAZIRI MPYA MAMBO YA NJE NA ULINZI

 

 

Kigali, RWANDA.

Rais wa Rwanda, Paul Kagame, amemteua Waziri mpya wa Mambo ya Nje na Ulinzi katika mabadiliko ya hivi punde kwenye baraza la mawaziri.

Hatua hii ya Rais Kagame imekuja, baada ya aliyekuwa waziri wa mambo ya nje, Louise Mushikiwabo, kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Muungano wa nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa (La Francophonie).

Kagame amemteua aliyekuwa katibu mkuu wa jumuiya ya afrika mashariki na mwanadiplomasia wa siku nyingi, Richard Sezibera, kuwa waziri mpya wa mambo ya nje.

Sezibera mwenye umri wa miaka 54, amerejea kwenye baraza la mawaziri baada ya awali kuwahi kuhudumu kama waziri wa afya.

Aidha, Jenerali wa Jeshi la nchi hiyo, Albert Murasira, kuwa waziri mpya wa ulinzi, anachukua nafasi ya James Kabarebe ambaye amekuwa akishikilia nafasi hiyo kwa muda mrefu.

Kabarebe ambaye anaonekana na wachambuzi wa siasa kama mtu mwenye ushawishi kwenye nchi za ukanda wa maziwa makuu, sasa atakuwa mshauri wa Rais Kagame kuhusu masuala ya usalama

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.