RAIS DKT MAGUFULI AISHUKURU SERIKALI YA UINGEREZA, WIZARA YA AFYA YASHUKIWA NA NEEMA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Magufuli ameishukuru Serikali ya Uingereza kwa kutoa misaada mbalimbali ikiwemo shillingi billioni 307.5 kwa lengo la kuunga mkono jitihada zake za kupambana na rushwa.

Rais Dkt, Magufuli Leo ametembelewa na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza Penny Mordaunt ambapo aliongozana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Sarah Cooke pamoja na Mkuu wa ofisi ya DIFD nchini Beth Arthy.

Amesema kuwa fedha hizo zimelenga kusaidia mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kuboresha Sekta ya Elimu pamoja na Sekta ya Afya ambapo kati hizo Shilingi Bilioni 160 zitaenda katika sekta hiyo lengo la kununua vifaa mbalimbali ikiwemo madawa.

Aidha amesema, katika Mpango wao wa mwaka wa fedha 2018/ 19 tumeamua kuongeza Bajeti ya Afya, kununulia Madawa kutoka Bilioni 31 hadi Bilioni 269, na hizo zinazokuja zitaenda kuimarisha masuala ya Afya.

“Tumeamua kuanza kujenga vituo vya Afya, vitakavyokuwa vinafanya kazi operation zaidi ya vituo 208, zaidi ya hospital za wilaya 67 na kununua vifaa na Madawa na kujenga hadi viwanda vinavyohusiana na kutengeneza Madawa”

Ameongeza kuwa, katika Njia hii Waziri wa masuala ya maendeleo wa Uingereza amekuja kutueleza kuwa katika zile zingine zinazobaki kati ya 307.5, Zaidi ya Bilioni 160 zielekezwe kwenye masuala ya Afya.

Aidha amesema Serikali imetenga zaidi ya shillingi billioni 124 kwa ajili ya kutekeleza elimu kwa lengo la kumsaidia zaid mtoto wa kike pamoja na Walemavu

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.