RAIS AL BASHIR ABANWA VIKALI NA WASUDANI, WAAMUA KUANDAMANA KWA MAMIA MJINI KHARTOUM

Khartoum, SUDAN.

Maandamano makubwa yamefanyika mwisho wa mwaka 2018 katika mji mkuu wa Sudan Khartoum yakiitikia wito wa baadhi ya vyama vya upinzani na jumuiya za kiraia kwa ajili ya kulalamikia ughali wa maisha na hali mbaya ya uchumi wa nchi hiyo.

Waandamanaji hao walikuwa wakielekea katika Ikulu ya Rais mjini Khartoum wakati walipokabiliwa na vyombo vya usalama vilivyolazimika kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji hao waliokuwa wakipiga kelele dhidi ya serikali ya Rais Omar Hassan al-Bashir.

Waandamanaji wengi walikuwa wamebeba mabango na maberamu yenye maandishi yasemayo ‘Irhal’ yaani ondoka yakimtaka Rais Omar Hassan al-Bashir wa nchi hiyo aachie ngazi na kuondoka madarakani.

Maandamano ya mkate ambayo yamekuwa yakishushuhudiwa nchini Sudan kwa zaidi ya wiki moja sasa na ambayo yamechukua mkondo wa kisiasa, yamezidi kuigubika nchi hiyo na kuifanya serikali ya Rais Omar Hassan al-Bashir ikabiliwe na mashinikizo zaidi.

Kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty Internatioanal, hadi hivi sasa watu wasiopungua 38 wameshauliwa na maafisa usalama wa serikali ya Rais Omar al Bashir, ingawaje serikali yenyewe inashikilia kuwa watu waliouawa ni 19.

Wakati huo huo, Rais Omar Hassan al Bashir wa Sudan amesema kuwa, kwa kudhibiti hali ya kiuchumi nchi hiyo inaweza kuondokana na mgogoro wa sasa na kwamba matukio ya wizi na uporaji kunaifanya hali ya mambo kuwa mbaya zaidi na si suluhisho la matatizo ya kiuchumi yanayoikabili nchi hiyo.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.