RADI YAUA MKAZI MMOJA MKOANI LINDI

 

Na Mwandae Mchungulike,Lindi

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Salima Ali Kolela (45) amefariki dunia jana desemba 3 baada ya kupigwa na radi akiwa nyumbani kwake katika kijiji cha Mbuli kata ya Kichonda wilayani Liwale mkoa Lindi.

Jabili Mpako ambaye mume wa marehemu amesimulia jinsi tukio lilivyotokea amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 10 jioni wakati yeye anatengeza msala mara baada ya mvua kunyesha waliingia ndani aliporudi tena mlangoni mke wake ambaye marehemu alikuwa amembeba mtoto ndipo radi ilipompiga na kumtupa nje na kuanguka na kupoteza fahamu.

Mwenyekiti wa kijiji cha Mbuli Ibrahimu Milango alisema alipata taarifa ya tukio hilo ni saa 12 jioni alipofika eneo la tukio aliwakuta wahusika wameelekea hospitali ya wilaya ya Liwale.

Kwa upande wake Kaimu mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Liwale,Dk Edwin Chavala amekiri kupokea mwili wa marehemu Salima Ali Kolela baada ya kufanyiwa uchunguzi wa awali amesema alishafariki lakini ahakukuwa na majeraha yoyote na kusema kuwa awenda alikuwa kwa mshituko wa sauti au mwanga wa radi.

Kaimu mganga mkuu amesema watu wanatakiwa kuchukua taadhali kuepuka kukaa chini ya miti mikubwa

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.