POLEPOLE:CHADEMA ACHENI MATUSI NA KUTUMIA VIONGOZI WA DINI KWENYE KAMPENI

John Marwa@darmpya.com

Dares Salaam

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimesikitishwa sana na kitendo cha viongozi wa dini kufanya kampeni za kumnadi mgombea wa CHADEMA, tena kiongozi huyo akatoa lugha chafu dhidi ya mgombea wetu wa CCM.

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu mwenezi wa Chama hicho, Hamphrey Polepole wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwendendo wa kampeni kufutia uchaguzi wa marudio wa majimbo na kata .

Amesema kuwa, wao kama chama tawala hawawezi kutumia dini kwenye majukwaa yao maana tunaheshimu sheria inayokataza mambo hayo na chama chao si cha mlengo wa kidini

Aidha ameitaka Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wawamulike Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jimbo la Monduli, kwani wanauthibitisho wa chama hicho kugawa rushwa ya chumvi nyumba kwa nyumba.

“Tunawaomba Takukuru wawaangalie Chadema jimbo la Monduli kwani wanatoa rushwa kwa kuwapa watu chunvi nyumba kwa nyumba na kwa bahati mbaya anayeongoza kugawa rushwa hii ni mgombea wao wa mwaka 2015″amesema Polepole

Amesema kuwa, Chadema wamepeleka watu kutoka sehemu mbalimbali nchini kwa ajili ya kuwatisha akina mama ili wasijitokeze kwenda kupiga kura, kwani wamegundua akina mama wameonekana wanaielewa CCM kwa sababu imewaletea mikopo nafuu.

“Chadema wamekua na njama nyingi dhidi ya CCM sasa hivi wameelekea upande wa akina mama kuhakikisha hawapigi kura, hawamchagui kiongozi wanaemtaka, hivyo tunavitaka vyombo vya dola kuthibiti hawa wahuni ” amesema Polepole.

Hata hivyo, amesema anamshauri Lowassa akalee wajukuu, hapendi kumuona anastaafu siasa kwa fedheha, sisi chama cha Mapinduzi tulikuwa tunamsubiri huyu Lowassa ampeleke mtoto wake Fred ili tumyooshe.

“Lowassa alikuwa amejimilikisha jimbo la Monduli, watu wa Monduli hawamilikiwi na mtu na tunakwenda kurudisha heshima ya Komredi Sokoine wilayani Monduli ” amesema Polepole.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.