PATORANKING KUKINUKISHA DAR LEO

Dar es Salaam

Mkali wa muziki kutoka Nigeria Patrick Nnaemeka Okorie, maarufu kama Patoranking ametua bongo kwa ajili ya kufanya tamasha kubwa linalotarajiwa kufanyika leo jijini Dar es salaam.

Akizungumza na wanahabari mkali huyo wa Nigeria amesema kuwa amefurahishwa kurudi Tanzania kwa mara nyingine kufanya tamasha kubwa ambalo ameahidi kufanya tamasha ambalo halijawahi kufanyika bongo na msanii wa nje.

Naye mkali wa bongo fleva Chege Chigunda amewashukuru waandaaji wa Tamasha hilo kwa kumchagua yeye kuwa mmoja ya wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo kubwa la muziki.

Tamasha hilo lililoandaliwa na Buckets na Hugo domingo LTD litakalofanyika katika ukumbi wa Buckets,Masaki pia litatumbuizwa na mkali kutoka kiwanda cha bongo fleva Quick Rocker (switcherBaba)Chege Chigunda na Grace kuanzia saa mbili usiku.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.