WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 30 JELA KWA MAKOSA MBALIMBALI.

  Mpwapwa -Dodoma. Mahakama ya Hakimu mkazi ya wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma imewahukumu kifungo cha miaka thelathini bwana Leonard Chande (42)Job Chisuche(18)na Kulwa Mathayo (19)wakazi wa Chinyika na Mkanana baada ya kupatikana na hatia ya kulima Bangi na imemuhukumu miaka 30 jela na kuchapwa viboko 12 Anton Paroweya mkazi wa Bumira baada ya kupatikana na hatia ya kubaka . Wakati huo huo mahakama hiyo imemuhukumu kifungo cha miaka Saba bwana Mbezwa Chilongani kwa tuhuma ya shambulio na kujeruhi. Kesi hizo zote zilizo kuwa zinasikilizwa na hakimu mkazi bwana Pascal…

Soma Zaidi >>

DC NEWALA, KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WAKABIDHI MAGHALA YA KOROSHO KWA JWTZ.

  Baada ya faraja waliyoipata wakulima wa zao la Korosho wilayani Newala pindi Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipotangaza Korosho yote Kununuliwa kwa Tsh. 3,300 imekuwa ni furaha na nderemo kwa wakulima wa korosho. Mkuu wa Wilaya ya Newala Mhe. Aziza Mangosongo ameendelea na zoezi la kuwaonyesha na kuwakabidhi maghala yote yaliyomo ndani ya Wilaya ya Newala Jeshi la Wananchi Tanzania kwa lengo la kuendelea na kazi yao kwa upande wao. Aidha Mhe. Mkuu wa Wilaya Newala amempongeza Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maamuzi ya kununua…

Soma Zaidi >>

TUNAPASWA KUWA MABALOZI WAZURI WA LISHE KWA VITENDO NA SIO KWA MANENO TU.

  Hayo yamesemwa leo na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg. James Mkumbo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya wakati akifungua semina ya Lishe wilayani hapo. Semina hiyo ya siku moja ambayo inaendeshwa na Tamisemi kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa ilihudhuriwa na baadhi ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo ambaye pia ni diwani wa kata ya Ubungo Mhe. Boniface Jacob, wakuu wa idara ambao wanahusika moja kwa moja na masuala ya lishe na mtaalam wa lishe kutoka Tamisemi Bi. Mary Kubona na Afisa lishe wa mkoa Bi.…

Soma Zaidi >>

MBUNGE WA TEMEKE AWAHI KABLA YA DIRISHA LA USAJILI CCM KUFUNGWA,ATANGAZA KUJIUZULU.

Na Bakari Chijumba Mbunge wa Temeke Abdallah Mtolea ametangaza kujiuzulu nafasi ya Ubunge na kujivua nyazifa zake zote ndani ya chama chake cha CUF akidai kuwa ni kutokana na mgogoro uliomo ndani ya chama hicho. Mtolea Ametangaza uamuzi huo leo bungeni mjini Dodoma na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge, licha ya kwamba bado hajaweka wazi kama anahamia chama kingine ingawa amesema yuko tayari kujiunga na chama chochote nje ya CUF. Maamuzi ya Mtolea yanakuja ikiwa imepita siku moja tu tangu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitangaze rasmi kuwa Leo kunafunga…

Soma Zaidi >>

ORODHA YA MAWAZIRI NA WABUNGE WENYE MAHUDHURIO HAFIFU BUNGENI YATAJWA.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, amewataja wabunge na mawaziri wenye mahudhurio hafifu zaidi katika vikao vya kamati za bunge na bungeni. Spika Ndugai,amewataja mawaziri hao na wabunge Leo bungeni jijini Dodoma mara baada ya kumalizika kwa kipindi Cha maswali na majibu. Spika huyo amesema orodha hiyo inatokana na mahudhurio ya wabunge na mawaziri kwenye mkutano wa 11 kuanzia Bunge la Bajeti pamoja na mkutano wa 12. Mhe.Ndugai ametaja orodha ya mawaziri hao ni pamoja na Waziri Lukuvi (Ardhi,Nyumba na Maendeleo na Makazi) asilimia 40,…

Soma Zaidi >>

MTOTO WA MIAKA (8) ACHOMWA KISU BAADA YA KUVUNJA CHUPA.

Mtoto aliyefahamika kwa jina la Zainabu Hussein (8) amechumwa kisu na mama yake Ashura mkazi wa Tanga baada ya kuvunja chupa ya chai. Akisimulia tukio zima Mtoto Zainabu alisema kuwa kabla ya mama yake kuchomwa kisu kilichowekwa kwenye moto alichapwa viboko kwa sababu aliangusha chupa ya chai. “Siku ya Jumamosi mama Ashura alinichapa na kisha kunichoma na kisu ambacho alikuwa amekiweka kwenye moto kwa sababu nilikuwa nimebeba chupa ya chai kwa bahati mbaya ikaanguka na kupasuka ndiyo mama akanipiga halafu akachukua kisu na kukiweka kwenye moto kisha akaanza kunichoma nacho…

Soma Zaidi >>

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUFANYA ZIARA YA SIKU MOJA NACHINGWEA.

  Na, Bakari Chijumba. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa, anatarajiwa kutembelea Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi, Jumamosi ya tarehe 17, Novemba 2018. Taarifa iliyotolewa hii leo Novemba 15, na Mbunge wa Nachingwea, Mhe. Hassani Masala inasema kuwa, Mhe. Waziri mkuu atatua uwanja wa ndege wilayani Nachingwea mnamo saa mbili asubuhi akitokea Dodoma na kupokelewa na Mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Rukia Muwango pamoja na viongozi wengine wa serikali, kisha Waziri atafanya ziara ya siku moja katika wilaya hiyo kwa kutembelea tarafa ya kilimarondo. ”…

Soma Zaidi >>

SHULE SUN ACADEMY ENGLISH MEDIUM IRINGA WAJIPONGEZA KUFANYA VIZURI ….

Na Francis Godwin,Iringa UONGOZI  wa    shule ya Sun Pre  & PRIMARY English Medium mkoani  Iringa  umewapongeza  wafanyakazi  wake  wakiwemo  walimu  kwa kuiwezesha shule  hiyo   kushika nafasi ya juu matokeo ya darasa la saba kitaifa. Mkurugenzi mtendaji  wa shule  hiyo  Edward  Nguvu  Chengula amesema  amelazimika kuwaandalia  sherehe maalum  ya  kuwatoa  nje ya  mji  wa Iringa wafanyakazi wake  kama sehemu ya  kuwapongeza  na  kujipongeza kwa  kuiwezesha shule hiyo  kuendelea  kufanya   vizuri . Chengula  alisema  matokeo mazuri ya  shule  hiyo  yamepelekea   wazazi  wengi  kutoka ndani ya mkoa na nje ya mkoa wa Iringa  kuhamisha …

Soma Zaidi >>

MKUU WA IDARA YA VYUO VIKUU UVCCM AZUNGUMZA NA VIONGOZI SENETI MKOA NA MATAWI.

  Dodoma. Mkuu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu Umoja wa vijana Chama cha Mapinduzi leo Novemba 14, 2018 amefanya mazungumzo na viongozi wa seneti Mkoa na viongozi wa matawi yote jijini Dodoma. Ndg. Khamana Juma Simba amewapongeza viongozi hao kwa kazi nzuri wanazozifanya lakini pia amewaagiza viongozi wote kuwa wana wajibu wa kudumisha Umoja na ushirikiano kuanzia ngazi za matawi,wilaya na Mkoa  na hasa katika maeneo husika ili kuimarisha Chama cha Mapinduzi. Pia amewaomba wanavyuo kushirikiana na umoja wa vijana kwa kwa lengo la kutengeneza umoja baina ya…

Soma Zaidi >>