ORODHA YA MAWAZIRI NA WABUNGE WENYE MAHUDHURIO HAFIFU BUNGENI YATAJWA.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, amewataja wabunge na mawaziri wenye mahudhurio hafifu zaidi katika vikao vya kamati za bunge na bungeni.

Spika Ndugai,amewataja mawaziri hao na wabunge Leo bungeni jijini Dodoma mara baada ya kumalizika kwa kipindi Cha maswali na majibu.

Spika huyo amesema orodha hiyo inatokana na mahudhurio ya wabunge na mawaziri kwenye mkutano wa 11 kuanzia Bunge la Bajeti pamoja na mkutano wa 12.

Mhe.Ndugai ametaja orodha ya mawaziri hao ni pamoja na Waziri Lukuvi (Ardhi,Nyumba na Maendeleo na Makazi) asilimia 40, Luhaga Mpina (Uvuvi na Mifugo) asilimia 45, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi (38%),Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga (35%) na Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira, January Makamba (37%).

Akitaja maudhurio ya wabunge spika Ndugai amesema wabunge wa mwisho kabisa na mahudhurio yao kwenye mabano kuwa ni Mbunge wa Jimbo la Mpendae (CCM), Salim Turki (14%), Mbunge wa Kishapu (CCM), Suleiman Nchambi (9%) na Mbunge wa Arusha mjini (Chadema), Godbless Lema (7%).

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.