NIMEMPA KICHAPO NDIO …………

Mama mzazi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Bi. Sandra au maarufu kama Mama Diamond amethibitisha kumpa kipigo cha mbwa mwizi mkwe wake Hamisa Mobetto.

Mwanzoni mwa wiki hii kuna stori ilisambaa kuwa Mama Diamond kampa kipigo kizito Hamisa baada ya kuwepo nyumbani kwa Diamond Madale, hadi kuacha wigi lake.

Mama Diamond amethibitisha habari hizo kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers ambapo ameweka wazi kuwa hampendi na hataki hata kumuona nyumbani kwake:

“Ni kweli nilimpiga na wigi nikamvua na hayo mambo ya kumfuata mzazi mwenzie ni huko, pale Madale ni kwangu na simtaki nyumbani kwangu kabisa.

Mama Diamond aliulizwa sababu gani hasa ilimfanya amchukie Mobetto na alifunguka haya:

Kitendo cha kuniitia mimi Shilawadu (kipindi cha udaku cha Televisheni ya Clouds) kilinikera sana halafu nikaanza kutukanwa kwenye mitandao ya kijamii.

Lakini pia Mama Diamond aliweka wazi kuwa baada ya kumtembezea kipigo Hamisa alimvua wigi ndipo Diamond alikuja kumuamulia.

Mama Diamond ameweka wazi hamtaki Mobetto na kama mwanaye atakuwa na mahusiano naye basi hawataelewana.

Kwanza tu siyo mwanamke wa kuoa (wife material) hajui kutandika hata kitanda wala kufanya tu usafi ni shida.

Yaani atajua yeye mwenyewe maana mimi ndiyo nimemzaa Diamond na siyo yeye sasa sijui nani ana nguvu hapo.

Siwezi kukanyaga kwenye harusi yao hata siku moja watasherekea wenyewe”.

Mama Diamond ameweka wazi kuwa anataka Mwanaye amletee mwanamke mwingine anayejiheshimu na sio Mobetto.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.