NAIBU WAZIRI WA MAJI AKIRI KUSUASUA KWA MIRADI YA MAJI

Na Mwandae Mchungulike,Lindi.

Naibu waziri wa maji na umwagiliaji Mheshimiwa Juma Aweso amesema moja ya mpango mkakati wa upatikanaji wa maji ni kuanzishwa wakala wa maji vijijini.

Akizungumza mkoani Lindi leo asubuhi kupitia kituo cha radio Mashujaa Fm,Mh.Aweso amesema moja ya kazi ya wizara yake ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji.

Wizara ya maji na umwagiliaji lazima kuanzishwa kwa wakala wa maji vijijini mpango huu utasaidia endapo utasimamiwa vizuri.

Aidha Aweso amekiri kususua kwa mradi wa maji wa Ng’apa uliopo mkoani Lindi kwa kusema kuwa mradi huo ulikosewa kwenye kumpata mkandarasi.

Pia Aweso amewaomba radhi wananchi wa Lindi kwa kutokea kwa changamoto kwenye mradi huo wa Ng´apa na kuwaahidi mradi huo utakamilika.

Naibu waziri huyo amesema kuwa kwenye mradi wa maji Ng’apa maji yapo ila tatizo lililopo ni suala ya kimtandao lakini wizara yake watachukua hatua ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji.

Ikumbukwe kuwa mradi wa maji wa Ng’apa umemaliza fedha nyingi ambapo mpaka sasa haujakamilika.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.