NAIBU WAZIRI MHE. HASUNGA AHAMASISHA WAKULIMA KWA KUTEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII

 

 

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga amewashauri wakulima wajenge utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini mara baada ya kumaliza shughuli za mavuno.

Aidha, amewahamasisha wakulima hao mara baada ya kuvuna na  kuuza mazao yao watenge muda wa kupumzika kwa kutembelea maeneo tofauti na yale waliyoyazoea badala ya kukaa sehemu moja.

Ameitoa rai hiyo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wakati wa mkutano wa kilele cha  maadhimisho ya siku ya  chakula duniani iliyofanyika kitaifa katika mji wa Tunduma wilayani Mombo mkoani Songwe.

Amefafanua kuwa hata hapo zamani Mababu zao walikuwa wakifanya sherehe kubwa mara baada ya kuvuna mazao yao, hivyo Mhe.Hasunga  amewataka wakulima hao kuwa  pesa watakazozipata baada ya kuuza mazao wazitenge kiasi ili waweze kuzitumia  kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini badala ya wanaume walio wengi  ambao ni wakulima  kuzitumia pesa hizo kuongeza mke wa pili.

“Tengeni muda wa kula maisha, nendeni pale Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, nendeni kule Kimondo na kwingineko mkampuzishe akili ili mkirudi mnakuwa na ari mpya” amesema Waziri Hasunga.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.