NAIBU MKUU WA MAJESHI NCHINI COMORO AKAMATWA

Moroni, COMORO

Naibu Mkuu wa majeshi nchini Comoro, Kanali Ibrahim Salim, amekamatwa kuhusiana na uchunguzi kuhusu jaribio la njama dhidi ya Rais Azali Assoumani, kwa mujibu wa familia yake.

“Majira ya mchana siku ya jana Jumatatu, wanajeshi wawili walikuja na kibali wakimwomba Kanali Ibrahim Salim kufika kwenye kituo cha polisi kwa kesi inayomhusu kesi,

“Alirudi karibu saa 11 jioni, akabadilisha nguo na kuondoka. tulipata taarifa kwamba alikuwa amezuiliwa katika jela la Moroni.” Mshirika wake wa karibu ambaye hakutaja jina lake ameliambia shirika la Habari la AFP.

Kulingana na ndugu zake, Kanali Salim anazuiliwa jela kwa madai yanayohusiana na jaribio la njama na kitendo cha kigaidi dhidi ya serikali ya nchi hiyo.

Mwezi uliopita, mwendesha mashitaka wa Comoro, Mohamed Abdoua, alitangaza kukamatwa kwa watu watano, ikiwa ni pamoja na waandishi Said Ahmed Said Tourqui na ndugu wa makamu wa rais, katika kesi hiyo hiyo.

Mahakama pia imetoa waranti wa kimataifa wa kukamatwa dhidi ya makamu wa rais, Bw Dhaffar said Ahmed Hassane, katika kesi hiyo.

Kama upinzani, Hassane alipinga mageuzi ya hivi karibuni ya kikatiba ya Rais Assoumani, yaliyopitishwa Julai 30 kwa kura nyingi wakati wa kura ya maoni.

Mabadiliko haya yatamruhusu Azali Assoumani, kiongozi wa zamani wa mapinduzi ambaye alichaguliwa mwaka 2016, kutimiza mihula miwili mfululizo.

Assoumani tayari ametangaza nia yake ya kuitisha uchaguzi wa rais wa haraka mwaka ujao, na ikiwa atashinda atatawala nchi hiyo hadi mwaka 2029.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.