MWILI WA MWANAMAPINDUZI ALIYEJULIKANA KAMA KIBARAKA WA WAZUNGU “JONASI SAVIMBI” KUFUKULIWA NA KUPEWA HESHIMA KAMA BABA WA TAIFA HILO LA ANGOLA.

Jonas Savimbi.

Ni vyema na ni heshima kubwa pale viongozi wa Afrika wanapotambua mchango wa viongozi wao mbali na tofauti zilizowahi kutokea apo mwanzo sasa sikia habari hizi njema kutoka Angola.

Kiongozi wa UNITA Isaias Samakuva amedai kwamba amepewa nafasi hiyo na Rais wa Nchi hiyo Joao Laurenco kwamba Mwili wa aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini Angola Jonas Savimbi utafukuliwa kabla ya mwisho wa mwaka huu ili apate kupewa maziko mazui, kwa mujibu wa chama chake cha Unita kilichonukuliwa na shirika la habari la AFP na pamoja na Daily Nation .

Taarifa hizo zimetoka moja kwa moja LUANDA na imepitishwa na chama chake na kupewa ruhusa na Serikali kwamba Savimbi anapaswa Kuzikwa kwa Heshima kama mmoja wa wapigania Uhuru nchini Angalo kipindi Angola inatawaliwa na Ureno.

Savimbi aliuawa kwa kupigwa risasi zaidi ya 25 mwili na vikosi vya serikali ya Edward Das Santos ambapo katika risasi hizo 15 zilizama mwilini, tukio hilo lilokuwa Tarehe 22 Februari mwaka 2002 na kuzikwa siku iliyofuatia kama mzoga kwenye mkoa ulio mashariki wa Mexico (mekiko).

Wiki sita baadaye Unita walisaini makubaliana ya amani na serikali na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivuodumu miaka 27.

Kiongozi wa sasa wa chama cha Unita Isaias Samakuva, alitangaza kuwa mwili wa Savimbia utafukuliwa baada ya kukutana na Rais Joao Lourenco kwenye mji mkuu Luanda siku ya Jumatano.

Mapema mwezi huu aliilaumu serikali kwa kumnyima Savimbi maziko Mazuri hizi ni habari njema sana katika kuwaenzi viongozi wetu na kuweka tofauti zetu pembeni tunapaswa pia kuchukua kama mfano .

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.