MWENYEKITI NA MAKAMU WAKE KAMATI YA BUNGE YA BAJETI WAJIUZULU

DODOMA.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Hawa Abdulrahman Ghasia na pamoja Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jitu Vrajlal Soni wamejiuzulu nafasi hizo.

Katibu wa Bunge ndugu Stephen Kagaigai, akizungumza na mtandao wa Dampya.com hivi leo Agosti 28, 2018 amethibitisha taarifa hizo za kujiuzulu kwa viongozi hao katika kamati hiyo.

“Mpaka sasa hatujajua sababu za wao kujiuzulu lakini ni kweli wamejiuzulu nafasi zao.” amesema Kigaigai

Mh. Ghasia ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini (CCM) pamoja na Soni Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini naye CCM, wametangaza uamuzi wao huo leo asubuhi mjini Dodoma mbele ya wajumbe wa kamati hiyo.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.