MWENGE WA UHURU:MONDULI WAHAMASISHWA UFUGAJI KWA NJIA ZA KISASA.

Mwenge wa uhuru umetembelea Shamba la mifugo la Manyara (Manyara ranchi) lililopo wilayani Monduli mkoani Arusha ambapo kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Ndg:Charles Kabeho amewataka wafungaji kufuga kwa kutumia mbinu za kisasa ambazo hazi athiri mazingira na zenye kuleta tija kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Kabeho amesisitiza hilo mara baada ya kukagua shamba la mifugo Manyara ranchi lenye ukubwa wa ekari 45000 lililoanzishwa mnamo mwaka 1959 na muekezaji kutoka Ujerumani ambapo kwa sasa shamba hilo lilotolewa na serikali na kumilikishwa kwa wananchi wa vijiji vya Esilalei na Oltukai.

Katika taarifa maalumu ya shamba hilo iliyo somwa mbele ya mkuu wa wilaya ya Monduli, Idd Kimanta alie ambatana na kiongozi wa mwenge wa uhuru kitaifa bwana Charlse,Afisa mifugo huyo wa shamba la mifugo (manyara ranch) amesema kuwa lengo la shamba hilo ni kuboresha mifugo ya asili.

Aidha amesema malengo mengine ni sambamba na uhamasishaji wa ufugaji wa kibiashara kwa kutumia mbegu bora za mifugo aina ya Boran na kondoo na hatimae wananchi kujengewa tamaduni ya ufugaji wa kisasa ili kufungua mianya ya biashara nje ya mipaka ya Tanzania ikiwa ni juhudi za kuelekea nchi ya uchumi wa kati wa viwanda.

Kibiriti amesema Shamba hilo la mifugo lina thamani ya shilingi 501,130,000 ambapo shilingi 397,530,000 ni makadirio ya mifugo, huku gharama kwa upande wa miundombinu ikitajwa kufikia shilingi 103,600,000.

Katika shamba hilo lenye jumla ya ng’ombe 829, Kondoo 444 ambapo Afisa mifugo wa shamba la Manyara Lemaly Kibiriti imebainisha kuwa zaidi ya mifugo 1,273.

Mpaka sasa uongozi wa shamba la Manyara limetoa ajira 32 kwa wakazi wa vijiji vya Esilalei na Oltukai,huku uborashaji wa mifugo ya wenyeji kwa kutumia utaratibu uliowekwa unatumika vyema na kuleta matunda chanya ambapo kwa mwaka shamba hilo hutoa madume bora 20 kwa wananchi kwa gharama nafuu.

Amesema mitamba 200 ya wafugaji wa ndani na nje ya wilaya ya Monduli huku matunda ya shughuli za uzalishaji wa shamba hilo yakitajwa kuchangia maendeleo katika kijiji husika ambapo mpaka sasa tayari zahanati,mabwawa na madarasa kwa ajili ya jamii zinazo pakana na eneo hilo tayari zimesha jengwa ikiwa ni sehemu ya faida za shamba hilo kwa maendeleo ya kata hiyo.

Baadhi ya mifugo ya katika shamba la mifugo la Manyara linalomilikiwa na wanakijiji wa vijiji vya Esilalei na Oltukai kata ya Esilalei wilayani Monduli.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.