MWENGE WA UHURU WAWANUFAISHA WANANCHI WA KARATU.

Ikiwa ni siku ya pili tangu mwenge wa uhuru kupokelewa ukitokea mkoa wa Mara hatimae Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka amekabidhi Mwenge wa uhuru kwa mkuu wa wilaya ya Karatu Theresia Mahongo kwa ajili ya kuendelea na majukumu ya mwenge wilayani humo.

Baada ya kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Ndg:Charles Francis Kabeho kukamilisha ziara ya mwenge wilaya ya Ngorongoro ambapo katika wilaya hiyo amewaagiza wakuu wa idara ngazi ya wilaya na halmashauri kuwa na nidhamu ya fedha za maendeleo na kuhakikisha wanawashirikisha viongozi wengine katika changamoto za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kabla ya kujichukulia maamuzi ambao huenda yakaatarisha shughuli za utekelezaji wa maendeleo kama inavyo agiza ilani ya chama cha mapinduzi CCM.

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2018 Charles Francis Kabeho akisalimia na mkuu wa wilaya ya Karatu Bi Theresia Mahongo ambapo kitendo hicho kimetajwa kuashiria kupokelewa kwa kiongozi huyo kwa ajili ya kutembelea,kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo ya meendeleo wilyani humo.

Jumla ya miradi 6 ya maendeleo imezinduliwa na kiongozi huyo huku akibainisha kukosekana kwa mawasiliano na umakini juu ya matumizi chanya ya fedha za miradi ili kurahisisha zoezi hilo la ukaguzi na uzinduzi wa miradi.

Katika wilaya ya Ngorongoro Miongoni mwa miradi iliyozinduliwa ni pamoja na mradi wa vyoo chenye matundu 10,bweni la wanafunzi wa sekondari,maabara ya kisasa ya kemia na fizikia katika shule ya Nainokanoka,barabara ya kiwango cha changarawe kutoka Eneo la Errikepus mpaka Nainokanoka,mradi wa maji safi na salama pamoja josho la kisasa kwa ajili ya mifugo katiaka hiyo na vijiji jirani.

Mapema asubuhi ya leo Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa ndg. Charles Kabeho anatarajiwa kuzindua na kukagua maendeleo ya miradi zaidi ya 6 katika wilaya ya Karatu huku akiwa na mwenyeji wake mkuu wa wilaya ya hiyo bi Theresia Mahongo.

Kwa mujibu wa taarifa ya wilaya ya Karatu mwenge wa uhuru umepita kijiji cha Dofa na kuzindua mradi wa kilomo cha vitunguu katika shamba la bonde la Eyasi na kutembelea shamba la muekezaji mzalendo ndg Gilole katika kijiji cha Qang’ded.

Shamba la vitunguu ambapo kiongozi wa mwenge ametembelea baada ya uzinduzi wa mradi wa kilimo katika kijiji cha Qang’ded wilayani karatu.

Shamba hilo lenye zaidi ya hekari zaidi ya 70 limekuwa chachu ya kujiingizia kipato kwa wananchi ambapo kwa mujibu wa taarfa ya mradi huo zaidi ya wananchi 200 wamekuwa wakifanya kazi ndogo ndogo na kujipatia fedha kwa ajili ya kujikimu.

Aidha,Miradi mingine inayo tarajiwa kuzinduliwa na kukaguliwa ni pamoja na uzinduzi wa nyumba za walimu 6 kwa moja shule ya sekondari Baray,kuzindua kikundi cha vijana katika kampeni ya Tuwalinde vijana wetu,kufungua ofisi ya kijiji kwa ajili ya utoaji huduma,ukaguzi wa mradi wa maji katika kata ya Ganako,ukarabati wa kituo cha afya cha kambi ya Simba na zoezi litakalo ambatana na upimaji wa VVU bure kwa wananchi.

Kwa mujibu wa taarifa ya wilaya Karatu mwenge wa uhuru unatarajiwa kukesha katika viwanja vya mazingira bora kuashiria uzalendo wa wananchi ambapo kesho mwenge huo unatarajiwa kukabidhiwa katika wilaya ya Monduli kwa ajili ya kuendelea na ratiba ya mbio hizo za mwenge wa uhuru nchini.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.