MWAKITINYA AWANYOOSHEA KIDOLE WAPINZANI AMFAGILIA JPM

NA DANSON KAIJAGE, DODOMA

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM (NEC) Mussa Mwakitinya maarufu kwa jina la Mwana wa Mungu amewashambulia wabunge wa upinzani na kueleza kuwa wana nia mbaya na amani ya taifa.

Mwakitinya ambaye kwa mara ya kwanza amejitokeza hadharani na kuzungumza na vyombo vya habari amesema kuwa wanasiasa hao ni Mbunge wa Kigoma Mjini na Mwenyekiti wa Chama cha ACT -Wazalendo, Zitto Kabwe na mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.

Mnec huyo alisema kuwa wanasiasa hao wamekuwa wakifanya siasa za kulitia doa taifa kwa kulitangaza vibaya na kuwadhalilisha viongozi wakuu wa nchi.

“Nataka ni mwambie Zitto kuwa anatakiwa kurudi jimboni kwake kwa maana watu wake wanapata shida sana na nataka nikuambie Zitto kuwa hali mbaya sana jimboni,mimi ni Mnec nazunguka nchi nzima najua hali aliyonayo ya kisiasa “alisema Kitinya

Katika mazungumzo na waandishi wa habari Mwakitinya alimtaka Zitto kuacha kuendeleza siasa za ujumla na badala yake arudi jimboni kwake aka fanye sasa kwani bila kurudi jimboni hatarudi Bungeni tena.

Akizungumzia hali ya kisiasa ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu Chadema Mwakitinya alimtaka Lissu kurudi mapema jimboni na kama atachelewa atamkuta (Mwakitinya)akiwa mbunge wa Jimbo hilo.

Katika hatua nyingine Mnec huyo alisema kuwa anashangaa watu ambao wamekuwa na tabia ya kubeza Juhudi za Rais Dk John Magufuli.

Alisema hakuna kiongozi ambaye anaweza kumfikia Rais wa awamu ya Tano kwa kufanya kazi nzuri na zenye maendeleo kwa taifa na wananchi wake kwa ujumla.

Aidha alisema kuwa anazo taarifa za siri kuwa yapo baadhi ya mashirika ambayo yanawasaidia wanasiasa uchwara kufanya siasa chafu.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.