MRITHI WA MFALME SAUDIA ‘BIN SALMAN’ NI MBAYA ZAIDI KULIKO WATENDA JINAI.

 

Washington DC, MAREKANI.

Gazeti moja la Marekani la Foreign Policy limetoa changamoto kwa siasa za Marekani kuhusu Saudi Arabia na kuandika kuwa, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa nchi hiyo, Muhammad bin Salman ni mbaya zaidi kuliko watenda jinai wote Duniani.

Chombo hicho cha habari kimeashiria kuwa, jitihada zote zinazofanywa na baadhi ya maafisa wa serikali ya Marekani akiwemo Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi hiyo, Mike Pompeo, za kutaka kutetea mauaji ya Jamal Khashoggi aliyekuwa mwandishi na mkosoaji wa utawala wa Saudia na kusema, matamshi yaliyotolewa na Pompeo katika uwanja huo hayakinaishi.

Foreign Policy limeongeza kuwa, Pompeo ameutaja ukosoaji wa vyombo vya habari kuwa ni mashinikizo dhidi ya Bin Salman na amejaribu kupotosha kadhia mauaji ya Khashoggi ndani ya ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul kwa kuzungumzia masuala ya Iran.

Gazeti hilo la Marekani limeandika kuwa, baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani kusisitiza kuwa Saudi Arabia ni mshirika muhimu sana wa Washington, si ajabu tena kumuona akitetea jinai na mauaji yanayofanywa na watawala wa Saudi Arabia licha ya ukosoaji mkubwa wa jamii ya kimataifa.

Bw Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari aliyekuwa mkosoaji wa utawala wa Saudi Arabia, aliuawa kikatili kwenye ubalozi mdogo wa nchi hiyo mjini Istanbul Uturuki, tarehe 02 mwezi wa Oktoba na baadaye maiti yake ilikatwa vipande vipande na kupelekwa kusikojulikana. Saudi Arabia imekiri kwamba, maafisa wake walihusika na mauaji hayo.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.