“MKUU WA WILAYA YA KISARAWE MH. JOKATE MWEGELO KUJA NA MBINU MPYA ZA KUINUA ELIMU KISARAWE. “

Na..

Mwalimu Richard Augustine

Baruapepe: augustinerichard629@gmail.com

+255754728801.

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Bi JOKATE MWEGELO leo tarehe 23/08/2018 amefanya kikao wilaya Kisarawe katika ukumbi wa mikutano uliopo wilayani hapo chenye lengo la kuinua Elimu katika wilaya ya Kisarawe.

Akifungua kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe alianza kwa kuwatambulisha wadau mbalimbali walioamua kuunga mkono jitihada zake na jitihada za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wake Dr JOHN POMBE MAGUFULI ,alipongeza na kuwashukuru kwa kazi kubwa ambayo wameifanya ya kuamua kuleta baadhi ya vifaa mbalimbali ikiwemo Mashine ya kutolea nakala (photocopy machine) vitakavyotumika kusaidia na kurahisisha shughuli za kitaaluma mashuleni.

Mkuu wa wilaya alisema “Nawashukuru sana wadau wangu kwa kuja hapa Kisarawe kuungana nami katika kuhakikisha tunatekeleza ahadi zetu kwa kutoa mahitaji ya wanafunzi, hata hivyo niko tayari kupokea michango mingine kutoka kwa wadau mbali mbali ambao watakuwa tayari kushiriki na wanakisarawe katika kuwaletea Maendeleo.”

Pia mara baada ya Mkurugenzi wa wilaya ya Kisarwe kuwasilisha ripoti ya utendaji wa wilaya hiyo katika masuala ya Elimu Mkuu wa wilaya ya Kisarwe aliwapongeza wakuu wa idara pamoja na viongozi mbalimbali walioshiriki katika katika kipindi chote cha nyuma kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kitaaluma na kuifanya Kisarawe kupunguza idadi ya wanafunzi waopata daraja “O” kutoka wanafunzi 467 Mpaka wanafunzi 259 alisema;
“Idadi hii ni kubwa sawa na alimia 50 ya wanafunzi wote ambayo si jitihada ya kubezwa kwa viongozi wetu waliotutangulia, Leo nimeamua kukaa nanyi pamoja na viongozi wa idara mbalimbali kuwapongeza kwa jitahada zenu lakini tuanze na mkakati mpya kwa ajili ya kufanya vizuri kuanzia sasa.”
Sambamba na hilo Mkuu wa wilaya ya Kisarawe aliamua kuja na mipango ya utelekelezaji wa shughuli hii katika mkitadha wa aina kuu mbili ambayo ni mpango wa mda mfupi na mpango wa mda mrefu (LONGTERM PLAN AND SHORTTERM PLAN).
Katika kuhakikisha haya yanatekelezwa, Mkuu wa wilaya Bi JOKATE MWEGELO kwa kuanza na mpango mkakati wa mda mfupi; kwa wanafunzi wanaenda kufanya mitihani mwaka huu amesisitiza kuwa tutafute njia mbadala ya kuwafanya wanafunzi hawa kukaa shuleni mda wote na kuhakikisha wanatumia mda wa kutosha katika kujiandaa na mitihani yao ili tuweze kufikia azima na lengo letu la kuondoa “O”

Hata hivyo aliwasihi viongozi na wajumbe wote wa mkutano huo kuwa; kwa kushirikiana na wazazi/walezi, viongozi mbalimbali ,wadau wa Elimu na Jamii kwa ujumla kuwa watajikita zaidi kuwapa uelewa ili kuhakikisha wao kama sehemu ya Wanakisarawe wanashiriki kikamilifu katika kuungana na serikali yao ili kutoa urithi wa maisha kwa watoto wao.

Akizungumuzi pia suala la walimu wilayani kisarawe alisema;

“Tunatafuta namna bora kwa kipindi hiki kushirikiana na walimu ambao ndio wasimamizi wa wanafunzi wetu huko mashuleni kuwawezesha hasa kuwapa motisha walimu wote ambao shule na wanafunzi wao watafanya vizuri zaidi katika matokeo ya mitihani yao na hata walimu ambao watatumia mda wao wa ziada katika kuwasadia wanafunzi watakapo kuwa wanakaa mashuleni.”

Vilevile akizungumzia suala la utekelezaji wa mpango mkakati wa mda mda mrefu (LONGTERM PLAN)Mkuu wa wilaya ya Kisarawe akishirikiana na Mkurugenzi wa wilaya pamoja na DAS wa wilaya hiyo wamefanya tathimini wilayani humo na kubaini kuwa ili kufikia mafanikio ya kuinua Elimu lazima wajikite katika kuhakikisha Wanaboresha Miundombinu na Mazingira ya kujifunzia ikiwemo;Utengenezaji wa Madawati , ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na ofisi za Walimu, ujenzi wa matundu ya vyoo, ujenzi wa mabweni ya wanafunzi, ujenzi wa maktaba pamoja na Maabara kwa shule ambazo hazina maabara.

Aidha katika kuhakikisha haya yote yanatekelezwa na kufikiwa kwa wakati Mkuu wa wilaya ya Kisarawe aliwasihi na kuwaasa viongozi na wajumbe wote waliohudhulia kikao hicho akisema;
*“Ningependa tuwe na , umoja, upendo na mshikamano na kwenye kampeni kubwa kama hizi, viongozi na wakuu wa idara kushiriki kwa kutoa mawazo ili tukitoka tuwe kitu kimoja hasa katika masula yanayogusa vijana ili kuonesha kuwa Kisarawe imejipanga vizuri”*

Hata hivyo alisisitiza kwa kusema kuwa;
“Nitakuwa tayari kupokea , mawazo, maoni ,ushauri ,pamoja na mchango wowote kutoka kwa viongozi na wadau mbalimbali ili kuhakikisha kampeni kubwa ambayo anaianzisha inafanikiwa kwa kiwango cha juu zaidi”.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.