MKUU WA WILAYA YA KILOLO ASIA ABDALAH AWATAKA WAFUGAJI IRINDI KUJENGA NYUMBA BORA

 

Na Francis Godwin ,Darmpya Iringa

MKUU wa wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Asia Abdalah amewataka wafugaji jamii ya kimasai wakazi wa kijiji cha Irindi kuuza mifugo baadhi ili kujenga nyumba za kisasa.

Akizungumza na wananchi hao wakati alipofika kutoa pole kwa msiba wa mwanakijiji mwenzao aliyeuwawa na Tembo ,Mkuu huyo wa wilaya alisema faida ya ufugaji ni pamoja na wafugaji hao kuwa na makazi bora na sio kuishi katika nyumba zisizo lingana na Mali walizo nazo.

“Wengi wenu hapa mnaongoza kwa kuwa na ng’ombe nyingi zaidi ya 100 hadi 200 na kuendelea sasa kuna faida gani kuwa na mifugo mingi huku sehemu ya kulala huna ” alihoji Mkuu huyo wa wilaya ya Kilolo

Kuwa serikali imeendelea kusogeza huduma ya maji safi na umeme sasa kama wananchi hao hawatajenga nyumba bora huduma hizo zinaweza kuwapita kama hawataandaa mazingira mazuri ya kujenga nyumba za kisasa na kuachana na kuishi katika vibanda vya miti .

Alisema wafugaji hao wanaweza anzisha ushirikiano wa kuanza kujenga nyumba ya familia moja moja hadi wote watakapo kuwa na nyumba bora.

Pia alisema kupitia mifugo wanayofuga wanaweza punguza mifugo kwa kuuza ili kujenga nyumba.

 

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.