MKUU WA WILAYA YA KILINDI AKUTANA NA WAFANYABIASHARA NDOGO NDOGO NA KUTEMBELEA MRADI WA REA.

 

Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mheshimiwa Sauda Mtondoo hii leo ametembelea wafanyabiashara ndogo ndogo na kukagua mradi wa umeme wa REA.

Mhe. Sauda ameongozana na viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Makasini kupita kwa wafanyabiashara ndogo ndogo eneo la Kwediboma kwa lengo la kusikiliza kero zao na kuzitolea ufumbuzi.

Sambamba na kusikiliza kero za wafanyabiashara ndogo ndogo Mhe. Mkuu wa Wilaya aliweza kukagua mradi wa umeme wa REA uliopo Kijiji Cha Gombero katika kuhakikisha maagizo ya Waziri wa Nishati Mhe. Merdad Kalemani yametekelezwa tangu alipofanya ziara wilayani humo mnamo Octoba 8, 2018.

Mkuu wa Wilaya ya Kilindi aliongozana na Katibu Tawala wa Kilindi ,Kaimu Meneja Tanesco Wilaya ya Kilindi pamoja na viongozi wa kijiji cha Gombero.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.