MKURUGENZI MSD APIGIWA SIMU ‘LIVE’ KUJIBU HOJA JUU YA USAMBAZAJI DAWA DODOMA

Dodoma.

Serikali imesema kuwa kwa sasa hali ya upatikana wa dawa imeimarika na dawa muhimu zinapatikana kwa zaidi ya asilimia 90 katika hospitali, zahanati na vituo vya afya nchini.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Bw. Laurean Bwanakunu alipopigiwa simu na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, moja kwa moja kutoka studio za radio Nyemo FM ya jijini Dodoma, ikiwa ni muendelezo wa kuhakikisha wananchi wanapata majibu sahihi na ya haraka kutoka kwa watendaji wa serikali.

Akijibu hoja hizo, Bwanakunu ameeleza kuwa upatikanaji huo wa dawa unaenda sambamba na kupungua kwa bei za dawa baada ya MSD kutekeleza agizo la serikali la kununua dawa moja kwa moja kutoka viwandani badala ya kutumia mawakala.

Amesema kuwa MSD imeendelea kushawishi wawekezaji kuanzisha viwanda vya dawa hapa nchini ili kupunguza gharama za uagizaji dawa kutoka nje.

Bwanakunu ameongeza kuwa kwa sasa MSD inasambaza dawa kwa vituo mbalimbali vya upokeaji dawa vipatavyo 7514 na kutoa wito kwa vituo vya afya na hospitali kuagiza dawa mapema ili MSD iweze kuzisambaza kwa wakati.

Akiongea katika mahojiano hayo maalum, Dkt. Abbasi ameeendelea kusisitiza kuwa mageuzi yaliyotokea katika kipindi cha miaka mitatu ni safari muhimu ya kuelekea Tanzania yenye neema.

Akiongelea kuhusu zao la zabibu Dkt. Abbasi amesema kuwa Kwa sasa kumekuwa na hamasa ya kuhakikisha zao hilo linalimwa kisasa na kutosheleza ili kuvutia uwekezaji katika kujenga viwanda vikubwa zaidi vya mvinyo.

Aidha,ameeleza jinsi serikal ilivyoongeza kodi katika mvinyo wa nje ili kulinda zao hilo hapa nchini.

Katika majadiliano hayo Dkt.Abbasi amesisitiza kuwa vita ya kuhakikisha Tanzania inafaidika na rasilimali za madini aliyoianzisha Rais Magufuli imeanza kulipa kwani mapato ya madini yameongezeka kutoka chini ya TZS Bilioni 194 hadi TZS Bilioni 301 Juni, 2018.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.