MKANDARASI MUNGAI ASAIDIA YATIMA WA KITUO CHA DBL IRINGA.

 

NA FRANCIS GODWIN, IRINGA

Mkandarasi wa kampuni ya ujenzi ya GNSM Geofrey Mungai ametoa msaada wa chakula na nguo wa zaidi ya shilingi milioni 1 kwa watoto yatima wa kituo cha Daily Bread Life Tanzania (DBL) mkimbizi mjini Iringa kwa ajili ya kusherekea siku kuu ya Krismass na mwaka mpya.

Mungai amekabidhi msaada huo jana na kuwa amelazimika kutoa msaada huo kwa watoto hao kama njia ya kuwajali na kuwafanya yatima hao kufurahia sikukuu kama watoto wenye wazazi na sehemu ya kuhamasisha jamii kuendelea kuwakumbuka yatima wakati wa sikukuu na wakati wote.

Hata hivyo alitaka jamii kuendelea kuwakumbuka watoto hao yatima badala ya kuendelea kuwatenga na kuwanyanyapaa kwa madai kuwa watoto hao yatima hawakupenda kuwa yatima ila ni mipango ya Mungu na kuwa jamii kuendelea kuwabagua ni kuongeza unyanyapaa kwa watoto hao wasio na hatia mbele za Mungu.

Pia alisema kuwa kupitia kampuni yake ya ukandarasi mkoani Iringa amekuwa na kawaida ya kutenga bajeti kwa ajili ya kuwasaidia watoto wa kituo hicho cha DBL na vingine mkoani Iringa na kuwa ataendelea kufanya hivyo kwa kuwaweka jirani zaidi watoto hayo kama sehemu ya familia yake.

Aidha Mungai alipongeza jitihada kubwa zinazofanywa na uongozi wa kituo hicho katika kuwalea yatima hao na kuwa mbali ya kuwepo kwa vituo vingi vya yatima ila kituo hicho kimekuwa kikiwalea yatima hao kama familia na kuwa ni vigumu kuweza kuamini kama watoto hao ni yatima kutokana na maisha wanayoishi kituoni hapo.

Alisema jitihada mbali mbali zimekuwa zikifanywa na vionngozi wa serikali akiwemo Rais Dkt Magufuli kuona jamii yenye matatizo wakiwemo yatima hao wanapata zawadi mbali mbali kipindi cha sikukuu.

Hivyo aliiomba jamii kuiga mafano wa Rais katika kuwajali watoto yatima kwa kuwakumbuka wakati wa sikukuu mbali mbali .

mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho mchungaji Mpeli Mwaisumbe mbali ya kumpongeza Geofrey Mungai na familia yake kwa kutoa msaada huo pia alisema kuwa Mungai amekuwa bega kwa bega na kituo hicho .

Mchungaji Mwaisumbe aliwataka viongozi wa dini kufanya kai ya kuliombea Taifa pamoja na Rais Dkt Magufuli kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya badala ya viongozi wa dini kutumia nyumba za ibada kuishambulia serikali .

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na kupongeza jitihada za mkandarasi Mungai katika kuwaidia yatima bado aliwataka wananchi wa iringa kuendelea kutembelea vituo vya yatima na kuwasaidia .

kasesela alisema amekuwa jirani na kituo hicho cha yatima na vituo vingine wilayani Iringa na ataendelea kujitoa kwa ajili ya kuwasaidia yatima na wananchi wa Iringa kama sehemu ya majukumu yake .

Mkurugenzi wa kituo hicho Mchungaji Neema Mpeli akishukuru kwa msaada huo alisema kuwa jitihada zinazofanywa na mkandarasi Mungi katika kuwakumbuka watoto hao ni kubwa na kuwa amekuwa kiunganishi kati ya watoto hao na familia yake .

Alisema kuwa kituo hicho kina watoto zaidi ya 50 na wameendelea kusaidiwa na wadau mbali mbali na kutokana na jitihada za wadau hadi sasa kituo hicho kimefanikiwa na kuwa na shule ya sekondari kwa ajili ya kuwawezesha watoto hao kupata elimu ya sekondari na kuwa kwa wale ambao wanajhitaji kusaidia wanaombwa kutuma michango yao kupitia akaunti namba Benk ya Exim ni 5435526007 Daily Bread Life Childreans home, ama kwa njia ya M-PESA 0754362536.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.