MJUMBE WA UN KUMALIZA MZOZO BAINA YA YEMEN NA SAUDI ARABIA

Huko mashariki ya mbali mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Yemen, Martin Griffiths anatarajiwa kufanya zaira rasmi nchini Saudi Arabia na Yemen kufuatia mzozo uliopo baina ya matafa hayo mawili.

Griffiths Katika zaira yake hiyo, nchini Yemen anatarajiwa kukutana na Rais Abd Rabbo Mansour Hadi, baada ya kufanya mazungumzo na viongozi tofauti nchini Saudi Arabia.

Baada ya ziara yake nchini Saudi Arabia, atajielekeza nchini Yemen ambapo pia anatarajiwa kukutana na viongozi tofauti wa taifa hilo.

Saudi Arabia inaongoza jeshi la ushirika ambalo lilianzisha operesheni nchini Yemen mnamo Machi mwaka 2015 kuunga mkono serikali ya Yemen dhidi ya wapiganaji wa Houthis ambao wanaungwa mkono nao na Iran.

Hivi karibuni Griffiths kama msuluhishi aliyeteuliwa alifanya mazungumzo na kiongozi wa kundi la wapigananiji wa Houthis Abdelmalek al-Houthi, na baadae aliondoka mjini Sanaa Juma lililopita

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.