MILIPUKO NA MILIO YA RISASI YASIKIKA JIJINI NAIROBI, MAGARI YACHOMWA MOTO,WENGI WAJERUHIWA.

Na,Jovine Sosthenes.

Taharuki iliibuka jana mjini Nairobi kufuatia shambulio la milipuko na risasi inayosadikiwa kufanywa na magaidi katika eneo la 14 Riverside Drive, katika Hoteli ya Dusit D2 jijini Nairobi, Kenya na kusababisha vifo vya watu watano na kujeruhi wengine tisa.


Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Kenya, Shambulio hilo linadaiwa kutokea Januari 15,2019. Mda, saa 9 alasiri na kusababisha watu kadhaa kujeruhiwa huku magari manne yakichomwa moto na milio ya risasi ikidaiwa kusikika kutoka eneo la tukio.


Bado wahusika wa shambulio hilo hawajajulikana lakini askari wa Kitengo cha kudhibiti Ugaidi nchini humo (RECCE) na polisi wa usalama wa raia wameshawasili katika eneo la tukio kwa ajili ya kudhibiti hali hiyo na kufanikiwa kuwatoa watu waliokwama jirani na eneo la tukio.


Wahudumu wa Shirika la Msalaba Mwekundu walifika katika eneo hilo na kuendelea kuwasaidia kuwahudumia majeruhi wanaokimbizwa katika Hospitali ya Taifa ya Kenyatta mjini Nairobi, Avenue na Aga Khan huku majeruhiwa zaidi wakitarajiwa kupatika kufuatia shambulio hilo.


Wakati huo huo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Kenya, Inspecta Jenerali Joseph Boinnet amewataka wakenya kuwa watulivu.


Inadaiwa kuwa hadi muda huu, Polisi na vyombo vya usalama vya nchi hiyo vinaendelea na kukabiliana na washukiwa hao wa kigaidi ndani ya Hoteli ya Dusit D2, jijini Nairobi.
Wakati hayo yakiendelea mjini Nairobi, Kundi la Kigaidi la Al Shabab lenye makazi yake nchini Somalia limenukuliwa likidai kuhusika na shambulio lhilo ililotokea 14 Riverside Drive katika Hoteli ya Dusit, jijini Nairobi.


Kwa mujibu wa mitandao ya kijamii iliyomnukuu msemaji wa kundi hilo la kigaidi, msemaji huyo amedai bado wanaendelea kuwasiliana na wanaoendesha mashambilio hayo jijini Nairobi.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.