MIL. 250 ZA SHEIKH ZILIVYOMFIKISA MAHABUSU MENEJA WA DIAMOND ‘BABU TALE’

Meneja wa Mwanamuziki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz, Hamis Taletale maarufu kama Babu Tale amefikishwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam akiwa chini ya ulinzi kwa ajili ya kusikiliza kesi ya madai iliyofunguliwa mahakamani hapo na Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hamis Mbonde.

Babu Tale katika kesi hiyo yuko pamoja na ndugu yake Iddi Taletale  ambapo Mahakama hiyo iliwamuru kumlipa Sheikh Mbonde kiasi cha Sh. Milioni 250 baada ya kupatikana na makosa ya ukiukwaji wa haki za hakimiliki kwa kutumia masomo ya sheikh huyo kibiashara bila ridhaa yake kinyume cha sheria.

Katika kesi ya msingi, Sheikh Mbonde alidai kuingia mkataba na Kampuni ya Tip Top Connection ambayo Babu Tale ni Mkurugenzi wake, kwa ajili ya kurekodi mahubiri yake kisha wagawane mapato baada ya kuyauza.

Inadaiwa Babu Tale baada ya kuingia mkataba huo, walimuacha njia panda Sheikh huyo baada ya kurekodi mahubiri na kumueleza kwamba wameachana na mpango huo.

Babu Tale amewekwa mahabusu mahakamani hapo baada ya Naibu Msajili wa mahakama hiyo, Ruth Massam kuwapa muda wa dakika kumi pande zote zijadiliane jinsi ya kumaliza suala hilo.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.