MHE. MABULA AFADHILI VIFAA VYA MICHEZO VYENYE THAMANI YA SH. 6 MILIONI KOMBE LA MHANDU.

Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula hivi leo amekabidhi Vifaa Vya michezo vikiwemo Jezi, Mipira pamoja na Vitini Vya waamuzi vyenye thamani ya shilingi 6,000,000 kwa vikosi 11 kutoa Mitaa 11 ya Kata ya Mhandu vitakavyoshiriki michuano Kombe la Mhandu lililoandaliwa na Diwani Kata ya Mhandu Mhe. Constantine Sima litakalo anza mnamo tarehe 05.01.2019.

Mhe. Mabula akikabidhi Vifaa hivyo amewaasa wana Mhandu kutumia michuano hiyo kama fursa ya kufahamiana vyema na kuwa na umoja katika kuijenga Mhandu, sanjari uibuaji wa Vipaji itakayochochea Mpira wa mguu kuwa ajira na msingi wa maandalizi ya michuano ya ligi daraja la nne kupitia shirikisho la Mpira kwa wilaya ya Nyamagana NDFA linalotarajiwa kuanza March mwaka juu.

Naye Mhe. Constantine Sima Diwani Kata ya Mhandu amempongeza Mhe. Mabula kwa ufadhili huo kwa ngazi ya Mitaa itakayowezesha michuano hiyo kupata kikosi kimoja cha Kata.

Katika mashindano hayo mshindi wa Kwanza ataibuka na Ng’ombe, mshindi wa pili atapata Mbuzi watatu, na mshindi wa Tatu ataipata Mbuzi mmoja amesema Mhe. Sima.

Kadhalika Michuano hiyo itavikutanisha vikosi 11 kutoka Mitaa 11 ikiwemo Mtaa wa Mhandu, Kisiwani, Maswa Mashriki na Magharibi, Isegenhe A na B, Mahango, Sokoni, Temeke pamoja na Shigunga.

Hafla ya makabidhiano imehudhuriwa na Ndg. Said Kizota katibu mashindano ya NDFA, diwani Mwenyeji Mhe. Constantine Sima, Mwenyekiti wa taasis i ya First Community Organizations Ndg. Ahmed Misanga,Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Kata sanjari na uongozi wa vikosi vyote na wenyeviti wa mitaa.

 

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.