MGOGORO WA UUZAJI VIWANJA VYA KKKT WAMFIKISHA LUKUVI NJOMBE

Na Maiko Luoga Njombe.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.Willium Lukuvi Amewataka Watumishi wa Wizara hiyo Nchini kuwafikia Wananchi Katika Maeneo yao Ili kutatua Kero zinazowakabili Ikiwemo Kumaliza Migogoro ya Ardhi Inayowakabili Wananchi Kote nchini.

Waziri Lukuvi Ametoa Agizo hilo katatika Ukumbi wa Turbo Njombe Mjini wakati Akizungumza na Mamia ya Wananchi waliojitokeza katika Ukumbi huo na Kuwasilisha Kero zao Kupitia Program ya Funguka kwa Waziri Ambapo Baada ya Kuona Kero nyingi za Wananchi wa Njombe zaidi ya 300 Ndipo Mh. Lukuvi Aliamua kutoa Maagizo hayo kwa Wataalamu wa Ardhi Mkoani Njombe.

“Ndg zangu Wataalamu wa Ardhi niwaambie Kuwa sasa wote katika Idara hii ya Ardhi Mpo chini yangu Haijalishi wewe ni mpimaji au Mipango miji sasa wote Mpo kwangu Hivyo nahitaji Muwatumikie Wananchi wa Njombe Sio unakaa Ofisini halafu mimi nakuja Ndio nakutana na Kero nyingi kama hizi Kero zipo 393 Nyingi Sana Maafisa Ardhi Mnafanya Kazi Gani?? Au Mnataka hadi mimi nifike hadi huko Vijijini??.

Aidha Waziri Lukuvi Amesitisha Zoezi la Utoaji Hati katika Viwanja vinavyomilikiwa na Kanisa KKKT Diocess ya Kusini Kufuatia Mgogoro wa Ardhi Unaoendelea Kati ya Viongozi wa Dioces hiyo na Baadhi ya Waumini wanaopinga hatua ya Uuzaji Viwanja Vinavyomilikiwa na Kanisa Kwa Watu Binafsi kwaajili ya Makazi kwakuwa Mpango wa waumini wa KKKT Juu ya Viwanja hivyo vilivyopo katika Eneo la Nyekamtwe Ilikuwa ni Kujenga Chuo Kikuu Cha Kanisa.

Waumini hao walimweleza waziri Lukuvi kuwa Uongozi wa Kanisa Haukufuata Utaratibu wa Kuuza Viwanja hivyo kwakuwa Hawakutoa Taarifa kwa Waumini ili waridhie Uamuzi wa Kubadili Matumizi ya Eneo hilo na Kusema Kuwa Viongozi wao wanampango wa Kuuza Eneo hilo ili walipe Madeni ya Dioces waliyokopa Bila utaratibu.

Kwaupande wa Viongozi Akiwemo Askofu wa Kanisa Hilo la KKKT Dioces ya Kusini Askofu Isaya Japhet Mengele wamesema Kuwa wanamiliki Zaidi ya Ekari 1000 katika Eneo la Nyekamtwe Mjini njombe Hivyo Uongozi Kupitia Vikao halali na Mkutano Mkuu wa Sinodi Uliona nivyema Kugawa Nusu ya Ekari hizo Ili ziuzwe Kwalengo la Kukamilisha Ujenzi wa Chuo Kikuu cha Kanisa Hilo ambao tayari Umeshaanza kwakuwa Ekari hizo zinatosha Kukamilisha Taasisi hiyo.

Kufuatia Mvutano Huo Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Willium Lukuvi Ameuagiza Uongozi wa Kanisa Kuwasilisha Nyaraka zote kwa wakala wa usajili Lita ndipo zifikishwe kwake Ili Aweze Kujiridhisha Kisha Atatoa Kibali cha Kuendelea Kutoa Hati kwa Wananchi wanaonunua Viwanja hivyo kwa kuwa uongozi wa kanisa hilo haujavunja utaratibu kiserikali kama wanavyodai baadhi ya washarika.

Ziara hiyo ya Waziri Lukuvi Ni ziara ya Siku moja Mkoani Njombe Imehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoani Njombe pamoja na Serikali Akiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe Ndg. Jassel Mwamwala, Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Mkoani Njombe Ndg Fidelis Lumato, Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Njombe Pamoja na Wabunge wa Majimbo ya Makambako Mh. Deo Sanga (Jah people) Mbunge wa Jimbo la Lupembe Joramu Hongoli na Mh. Edward Mwalongo Mbunge wa Njombe mjini.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.