MEYA WA MJI NJOMBE AWAPIGA DONGO WAKAZI WA MJINI KWA KUTOA MICHANGO MIDOGO YA UJENZI

Na Amiri kilagalila

Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe Edwirn mwanzinga amewataka wananchi wanaoishi mjini kuacha tabia ya kukadilia na kutoa michango midogo isiyoweza kukamilisha miradi ya maendeleo kwa wakati hususani ujenzi wa madarasa ya shule kutokana na watoto wengi kushindwa kuanza masomo kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa.

Akizungumza na mtandao huu ofisini kwake amesema kuwa licha ya halmashauri yake kujitahidi kuwapeleka watoto wote katika shule mbali mbali hususani katika kata za vijijini kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa katika shule zilizopo katika kata za mjini, amewataka wananchi kuacha kuchangia michango kwa kiasi kidogo (4000) kwa kuwa kiasi hicho ni sawa na kwenda kuchangia jengo la choo wakati bado kuna uhitaji mkubwa wa ujenzi wa madarasa.

“kwa ujumla sisi hapa kwetu hakuna mtoto anayebaki bila kwenda shule, na watoto wote tumewapeleka katika kata zingine nadhani mpaka mwishoni mwa mwezi huu tutakuwa na madarsa ya ziada,lakini jitihada tunazotakiwa kuzifanya baada ya kukamilisha majengo haya tuliyonayo niombe kuwashauri wakazi wa mjini waache kuchangisha mchango kama unakwenda kujenga choo huwezi kuchangia shiringi 4000 wakati unakwenda kujenga madarasa 11 yatakwisha lini,wazazi wengi hawana shida ila wanafadhaika sana wanapoona watoto hawaendi shule na projection ya mwaka huu watoto zaidi ya 4000 watafaulu hiyo haikwepeki na kwasababu tumekwisha kujua lazima tuongeze nguvu hapa mjini haitakiwi tuwe na shida kwasababu kwanza tupo wengi na watoto wanazaliwa kila siku”Alisema Meya

Aidha halmashauri ya Mji wa Njombe Imetoa Shilingi Milioni 90 Kwa ajili ya Kusaidia Ujenzi wa Vyumba Vya Madarasa Kwenye Shule Zake za Sekondari Zilizokuwa na Upungufu wa Madarasa Uliosababisha Baadhi ya Wanafunzi Kukosa nafasi na kulazimika kuwasambaza watoto katika kata mbali mbali.

Halmashauri ya Mji wa Njombe Imefanikisha Kupasisha Jumla ya Wanafunzi 3001 Ambapo Kati Yao 572 Walielezwa Kukosa Nafasi Kutokana na Uhaba wa Madarasa Jambo Lililowalazimu Kuwapeleka Kwenye Kata Nyingine Ambazo Hazina Upungufu wa Madarasa.

Akizungumza Kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe,Afisa Elimu Msingi wa Halamshauri Hiyo Zegeli Shengelo Amesema Kuwa Tayari Madarasa Yameshajengwa na Yapo Katika Hatua za Awali na Kwamba Michango ya Wananchi Kwa Kushirikiana na Serikali Yenyewe Wametekeleza Zoezi la Ujenzi wa Vyumba Vya Madarasa Kwa Kiwango Kikubwa Kadri ya Maelekezo ya Waziri wa tamisemi Seleman Jafo.

“Baada ya kuona wanafunzi wengi wamebaki kwa kweli halmashauri imeona na kufanya jitihada za kuhakikisha wanafunzi wote wanaingia madarasani na mpaka dakika hii tumejenga vyumba 27 katika shule tofauti tofauti na”tuna uhakika siku hizi chache vitaanza kutumika” amesema Shengelo

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.