MEDDIE KAGERE APONGEZA USHIRIKIANO WA WACHEZAJI WENZAKE MSIMBAZI

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Simba Meddie Kagere amewapongeza wachezaji wenzake katika kikosi cha klabu ya simba kwa kumuonyesha Ushirikiano mzuri pasipo kujali Kitu chochote

Kagere ameeleza kwamba tangu aingie klabuni hapo amekuwa akijihisi kama yupo nyumbani kutokana na mapokezi mazuri aliyoyapata toka kwa Uongozi wa klabu , mashabiki na hata wachezaji wa klabu hiyo .”

Nafurahishwa na maisha ya hapa , Wachezaji wanaonyesha morali kwangu na nashirikiana nao Vizuri sana .kagame Cup ni mashindano yangu yangu ya kwanza nikiwa na simba SC lakini Wachezaji wameonyesha Ushirikiano mkubwa kwangu. ” – Alisema Kagere

Kagere ambaye alisajiliwa klabu ya simba SC toka klabu ya Gormahia ya kenya tayari ameitumikia klabu hiyo katika michezo miwili ya kombe la kagame na kufanikiwa Kufunga mabao 2

 

Kesho atakiongoza kikosi cha simba Katika mtanange wa hatua ya robo fainali ya mashindano hayo , ambapo Simba SC watavaana Uso kwa Uso dhidi ya klabu ya AS Ports toka nchini somalia majira ya saa 1:00 Usiku ndani ya Uwanja wa taifa . 

Related posts

One Thought to “MEDDIE KAGERE APONGEZA USHIRIKIANO WA WACHEZAJI WENZAKE MSIMBAZI”

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.