MCHUNGAJI TITO MWINGINE WA ZIMBABWE AKAMATWA NA POLISI KWA KUUZA TIKETI ZA KWENDA MBINGUNI

HARARE. Hakika Dunia ina mambo tena sana na binadamu katika enzi hizi hutumia kila mbinu kuhakikisha anavuna kutoka kwa mwenzake, huko nchini Zimbabwe Mchungaji mmoja amekamatwa na jeshi la polisi alipokuwa akiwauzia tiketi waumini wake akisema zitawawezesha kuingia mbinguni.

Pasta huyo aliyejulikana kwa jina la Tito Wats, pamoja na mke wake wamekuwa wakiwauzia kondoo wake tiketi za kwenda mbinguni kwa Dola 99.4 sawa na zaidi ya Tshs Laki Mbili na Elfu Ishirini. Kulingana na mchungaji huyo, Yesu alimjia binafsi na kumshauri aanze kuuza tiketi hizo.

Mbinu iliyotumiwa na mchungaji mmoja wa Zimbabwe kujichumia unga imewaacha wengi vinywa wazi kwani amekuwa akiwauzia kondoo wake tiketi za kuuona ufalme wa mbinguni.

Mchungaji huyo wa nchini Zimbabwe ambaye sasa mtandaoni amekuwa akizungumziwa sana, alikamatwa baada ya kujihusisha na tukio hilo. Polisi walilazimika kumkamata mchungaji huyo ambaye alidai kutumwa binafsi na Yesu kufanya kazi hiyo ili kuwaokoa watenda dhambi na moto wa jahenamu.

“Sijali wanachosema watu ama polisi kunihusu, nahukumiwa kwa kuwa nafanya kazi ya Mungu. Yesu Masiya alinijia na kunipa tiketi zilizotengenwezwa kwa dhahabu tupu ili niwauzie watu wanaotafuta uokovu”, alijitetea Mchungaji Tito wakati alipokuwa akihojiwa.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.