MBUNGE LUPEMBE APELEKA MABILIONI YA FEDHA JIMBONI KWAKE WAPIGAKURA WAELEZA.

Na Maiko Luoga Njombe

Wananchi wa Jimbo la Lupembe katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Mkoani Njombe Wamempongeza Mbunge wa Jimbo Hilo Mh. Joramu Hongoli Kwakile walichoeleza Kuwa Mbunge Huyo Anafanya Kazi kwa Umoja na Mshikamano na Wananchi wake Ikiwemo Kufika Mara kwa Mara Jimboni humo na Kusikiliza Kero zinazowakabili.

Wakizungumza na Mwandishi wetu Aliyetembelea Baadhi ya Kata jimboni humo Ikiwemo kata za Lupembe, Matembwe, Ikuna, Kidegembye Pamoja na Idamba Wananchi hao Walisema Kuwa Kupitia Msukumo na Ufuatiliaji wa Mbunge Huyo Tayari Serikali Kupitia Rais Magufuli Imetoa Fedha Kiasi cha Bilioni Moja na Milioni 500 Kwaajili ya Ujenzi wa Hospital ya Halmashauri Hiyo Inayojengwa Katika Kata ya Matembwe.

Aidha Wameeleza Kuwa Kupitia Mbunge Hongoli Serikali Imetoa Fedha za Kitanzania Zaidi zaidi ya Milioni 150 Katika Kata ya Mfriga Wilayani Humo kwaajili ya Ujenzi wa Nyumba Sita za Walimu Ambazo Tayari zipo katika Hatua ya Ukamilishaji Jambo Ambalo wananchi wamesema Kuwa Serikali ya Awamu ya Tano Inawasaidia Kutatua Changamoto katika Jamii Ikiwemo Kuboresha Miundombinu ya Elimu katika Maeneo yao.

“Tunamshukuru Sana Rais wetu Magufuli Ametusaidia sisi Watu wake wa hali ya chini Ameleta Pesa za kujenga Hospital kubwa, Maji pamoja na Nyumba za Walimu Haya ni mambo ambayo Serikali Ingetuachia Sisi wananchi Peke yetu Tusinge weza Kukamilisha tena Tungejenga Majengo ya Kienyeji Pia Tunaambiwa Tutajengewa lami kutoka Kibena kupitia Hapa Lupembe hadi Madeke Kuunganisha na Mkoa wa Morogoro Hili ni jambo jema Sana Tunaomba na Mbunge wetu Mh. Joramu hongoli Aendelee kutusaidia”.Walieleza Wakazi wa Lupembe.

Bw. Valentino Aidan Hongoli Ni Diwani wa Kata ya Ikuna Pia Ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Amesema Kuwa Baadhi ya Vijiji katika Halmashauri hiyo Vinakabiliwa na Changamoto ya Maji Ikiwemo Kijiji Cha Kidegembye Hivyo Serikali Imekamilisha Mradi Mkubwa wa Maji katika Kijiji hicho Uliogharimu Kiasi cha Bilioni Moja na Milioni 300 Pesa za Kitanzania Mradi Ambao wananchi Wataanza Kupata Huduma ya Maji Siku Chache Zijazo Hata hivyo Mchakato wa Kuboresha Huduma hiyo ya Maji Unaendelea Katika Vijiji Vingine Ikiwemo Mayembela na Lupembe.

Alisema Kwasasa Wananchi wa Halmashauri yake Wanasubiri kwa Hamu Kubwa Kuanza kwa Ujenzi wa Barabara ya Lami Ambayo imetajwa Katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM Barabara ya Kutoka Kibena, Lupembe Hadi Madeke Itakayounganisha Mkoa wa Njombe na Morogoro Maeneo Ambayo Wananchi wake Ni wazalishaji wakubwa wa Mazao mbalimbali ya Biashara Ikiwemo Matunda, Miti Na Viazi Mviringo Ambavyo Soko Lake ni La uhakika Ndani na Nje ya Tanzania.

“Kwakweli Ndg. Mwandishi Mimi niseme Kuwa Sisi wananchi wa Wilaya ya Njombe Tunaimani Kubwa Sana na Mh. Rais Magufuli Pamoja na Mbunge Wetu Ndg. Joramu Hongoli kama wameweza Kutuletea Fedha za Kujengea Hospital Kubwa ya Wilaya pamoja na Kuboresha Miradi ya Maji Tunaimani Pia Hii Barabara ya Kibena Kupitia Lupembe hadi Madeke Itajengwa kwa Lami na Uzuri wake hata Kwenye Ilani Imetajwa hivyo Serikali ya Rais Magufuli inaitambua Rasmi “. Alisema Mwenyekiti huyo wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.