MAVUNDE AKABIDHI GARI LA HUDUMA ZA MAZISHI,WANANCHI DODOMA MJINI WAMPONGEZA

Dodoma.

Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Mheshimiwa Anthony Mavunde leo ametekeleza ahadi yake ya kuwapatia wananchi wa jimbo hilo gari la kuhudumia shughuli za mazishi ambalo litatumiwa na wananchi wote bila gharama yoyote.

Gari hilo maalum la huduma za mazishi limekabidhiwa leo kwa wananchi wa Dodoma chini ya uratibu wa ofisi ya mbunge na ofisi ya mkuu wa wilaya Dodoma mjini ambapo mbunge Mavunde amewashukuru wamiliki wa vituo vya G.88 NJOMBE FILLING STATION(NFS)na GAPCOkwa kujitolea mafuta lita 150 kwa mwezi kama sehemu ya mchango wa uendeshaji wa gari hilo.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr.Benilith Mahenge ambaye amempongeza mbunge Mavunde kwa jitihada kubwa ya kuwahudumia wananchi na kutaka wanachi hao kulithamini na kutoa ushirikiano kwa mbunge huyo.

Akishukuru kwa niaba ya Wazee wa Dodoma,Katibu wa Baraza hilo mzee Makuberi amempongeza mbunge Mavunde na kushangazwa na kasi ya maendeleo ndani ya muda mfupi katika jimbo la Dodoma mjini.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.