MAUZO DSE YAPOROMOKA

Mauzo ya Hisa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) yameshuka kutoka Sh bilioni 1.11 wiki iliyopita hadi Sh milioni 676.26 wiki hii.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Biashara na Masoko, Emanuel Nyalali, amesema mauzo hayo yametokana na kuuzwa kwa mihamala 166.

“Wakati huo thamani ya Soko la Hisa imeongezeka hadi kufikia Sh trilioni 22.18 kutoka Sh 21.99 wiki iliyopita,” amesema Nyalali.
Aidha amesema katika kipindi hicho, hatifungani za serikali na makampuni zenye thamani ya Sh bilioni 1.96 ziliuzwa kwenye mihamala 10.
Alisema mauzo ya hatifungani wiki iliyopita yalikuwa ya Sh bilioni 18.33 ziliuzwa kwenye mihamala 28.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.