MASWALI NA MAJIBU YA NAIBU WAZIRI MHE. ANGELINE MABULA KWENYE KUNDI LA TANZANIA YETU LA WHATSAPP

 

Na Dinna Maningo.

Baadhi ya Watanzania wamekuwa wakijiuliza maswali mengi juu ya maswala mbalimbali yanayofanywa na Serikali pamoja na changamoto kadhaa ndani ya jamii lakini maswali yao hukosa majibu kwakuwa hushindwa namna wanavyoweza kufikisha ujumbe kwa mamlaka husika.

Pia wengine utamani maswali hayo yangejibiwa na Viongozi wa Serikali wakiwemo Mawaziri wa Wizara mbalimbali lakini kutokana na mazingira ya kuwawezesha kuonana ana kwa ana na viongozi hao wanashindwa kufikisha kero zao ili zitatuliwe.

Kwa kutambua umuhimu wa uhuru wa mawazo kundi laTanzania Yetu kupitia mtandao wa Kijamii wa Whassap lililoanzishwa julai 20,2018 likiongozwa na mkuu wa kundi hilo Sitta Tuma wameona umuhimu wa kuwashirikisha wadau mbalimbali  kutoa elimu na kujibu maswali yanayoulizwa na wanakikundi.

Kikundi hicho chenye jumla ya wajumbe zaidi ya 240 wakiwemo baadhi ya Viongozi  wa Serikali hususani Mawaziri wa Wizara mbalimbali,Wanasiasa,Wafanyabiashara,Wajasiliamali,Waandishi wa habari,Wanasheria ,Viongozi wa Dini wanaotoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania na baadhi ya Watanzania walioko nje ya nchi upata fursa ya kujadili maswala mbalimbali na kuwauliza maswali viongozi wa Serikali.

Mkuu wa kikundi hicho cha Tanzania yetu ambaye kitaaluma ni Mwandishi wa habari utoa mada mbalimbali za majadiliano na maswali nakuwajulisha wajumbe ili kuchangia mawazo yao na kuuliza maswali kwa mamlaka husika na mamlaka hizo kupitia wasemaji wake wakiwemo Manaibu Waziri utoa majibu na elimu, na kupitia majibu hayo watu wanaelimika.

Novemba 25,2018 Mkuu huyo wa Tanzania yetu akatoa mada iliyohusu Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi iliyohoji je zoezi la upimaji ardhi limefanyika kwa ufanisi? je kupima na kumiliki hati inafaida yoyote kiuchumi? na Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba,Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akapata fursa ya kujibu na kutoa elimu kupitia maswali yaliyoulizwa na wajumbe.

Wajumbe wauliza Maswali.

Samwel Mwanga kutoka mkoani Simiyu.

Swali.  Maeneo ya Vijiji yamepimwa na wananchi wamepatiwa hati za        kimila,Naibu Waziri Je kwanini baadhi ya benki hawazikubali hati hizo ili kumwezesha Mwananchi kuchukua mkopo wa fedha Benk?

Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba,maendeleo ya Makazi Angelina Mabula.

Jibu. Nianze kwa kumshukuru Mungu kutupa uhai. Aidha nimshukuru sana Mhe Rais kuendelea kuniamini kumsaidia katika wizara hii.

Kuhusu mabenki kutopokea hati za Kimila naomba nijue ni benki gani kwakuwa tunazo benki zaidi ya 10 ambazo zinapokea hati miliki za kimila. Mashahidi wanaweza kuwa Halmashauri ya Babati, Mbinga na kwibgeneko zaidi ya bilioni 59 zilitolewa kwa dhamana ya hatimiliki za kimila.

Joseph Gorya kutoka mkoani Simiyu.

Swali.Lamadi tulikuwa na zoezi la kupimiwa viwanja na tukaambiwa tuchangie 60,000 kila kiwanja tukachangia wakaja wakatuwekea bikoni lakini hajui hatima ya hati zetu je unaweza kutusaidia ili kufahamu hatima ya hati zetu mkuu maana tumeisha wekewa bikoni?

Naibu Waziri Mabula.

Jibu.Lamadi vilipimwa viwanja 1,935 kati ya hivyo viwanja  520 vilimilikishwa baada ya wahusika kukamilisha malipo,mwamko wa uchangia maeneo ya Itongo,Kisesa sokoni ulikuwa mdogo sana ,malalamiko yalifika kwa mkuu wa mkoa ndiyo maana Mwenyekiti na Katibu wa kamati walisimamishwa.hivyo haki yenu mtapata tu pale utaratibu wa mkoa utakapokamilika.

Matiko Nyaiho kutoka Shinyanga.

Swali.   Kama nimejenga nyumba katika eneo ambalo halijapimwa nifanyeje ili niweze kupimiwa kiwanja changu?

Naibu Waziri Mabula.

Jibu.   Kama kuna zoezi la urasimishaji linaendelea waone viongozi wako wa mtaa watakusaidia kutatua tatizo lako kupitia kamati maalumu za upimaji katika mitaa yenu.

Ashura Jumapili kutoka Kagera.

Swali.   Naibu Waziri kuna baadhi ya maeneo Bukoba wananchi wemehamasishwa kuchangia laki 2 kwajili ya upimaji wa viwanja ili waweze kupatiwa hati miliki zoezi kama hili liliwahi kufanyika miaka iliyopita lakini wananchi hawakupimiwa wakati walilipa hali iliyosababisha kuibuka kwa madai ya viwanja vyao katika mradi wa upimaji wa viwanja 5000 ambao ulikuwa tofauti, nakusababisha wananchi kuwa na mashaka katika zoezi hill jipya je ni kweli wakilipa watapata hati miliki kwa wakati?

Naibu Waziri Mabula.

Jibu:   Suala la urasimishaji ni tofauti na upimaji wa kawaida,mradi wa Viwanja 5,000 ulikuwa na utaratibu wake,mradi uliingia doa nakumbuka kuna baadhi ya viongozi akiwemo meya wa Bukoba aliguswa,kama watu walichangia na hawakupimiwa wakati wa urasimishaji naomba mpeleke barua zenu ofisi zetu za kanda ili wafatilie.

Goryo,Swali:Mh Waziri kwanza nikupongeze kwa kumaliza tatizo la yule mama wa Bunda ambaye kiukweli mlifanya kazi ya Mungu maana kwa umri wa yule mama bila busara zenu asingeliweza kurudishiwa kiwanja chake swali langu kwako, je mnafanya jitihada gani kutatua migogoro mingine ya aina ya Mama Nyangeta wa Bunda maana watu wengi sana wananyanyaswa na maafisa aridhi na hawajui wafanyeje?

Naibu Waziri Mabula.

Jibu: Nakushukuru kwa pongezi zako,Kuhusu swali lako kama wizara hatuwezi kujua nani na nani wamedhurumika au wanahitaji msaada wa wizara mpaka wanapojitokeza kama bibi Nyangeta. Nawashauri watumie ofisi zetu za kanda watawasaidia tunao wataalamu mtu hahitaji tena kuja tena Wizarani.

Goryo,Mimi nahitaji mkopo wa nyumba je kuna masharti gani?

Naibu Waziri Mabula

Jibu:Unalipa 20 – 25%kama down payment baadae unakuwa unalipa kila mwezi kutegemeana na makubaliano katika mkataba.

Daniel Limbe kutoka mkoani Geita.

Swali:Itakumbukwa kuwa Serikali ilitoa maelekezo kwa wamiliki wa nyumba za kupanga   kutoza kodi kwa mwezi mmoja mmoja pamoja na kutopandisha kodi kiholela lakini hali hiyo imekuwa ikiendelea pasipo kutazama uwezo wa mpangaji,Je Serikali imeshachukua hatua gani kuhakikisha maelekezo hayo yanazingatiwa na kuondoa kero hiyo kwa wapangaji.?

Naibu Waziri Mabula.

Jibu:Wizara imeshaweka mkakati vizuri sasa hivi tuko kwenye maandalizi ya mswada kwa ajili ya kupeleka Bungeni ambao utawekwa taratibu zote za maswala ya Kodi,ujengaji holela wa nyumba,madalali,haiwezekani mtu umwombe pesa ya mwaka anaipata wapi nawakati analipwa mshahara kwa mwezi!.

Oscar Kaijage kutoka mkoa wa Shinyanga.

Swali:  Maeneo mengi ya mjini kuna kitu kinaitwa watu wazawa watu hawa ni wale wanaomiliki nyumba ambazo ni za zamani hazifai zimechakaa,je ni kwanini watu hawa wasipewe viwanja vingine nje ya mji na hivi vya mjini wakapewa watu wenye pesa zao ili kuendeleza miji?

Naibu Waziri Mabula.

Jibu:Siyo rahisi umtoe mtu mjini umpeleke nje swala la msingi kama wako mjini na nyumba zao zimechakaa na tayali mjini kuna mipango miji kipaumbele watatakiwa kujenga kwa mapango huo,kama hawezi basi ni maamuzi yake auze atoke au ampangishe  mtu kwa mkataba huwezi kumwamisha kisa tuu nyumba yake imechakaa ameshindwa kuiendeleza.

Sitta Tuma kutoka Mwanza

Swali.   Mhe. Waziri sheria ya mazingira inazuia mtu yeyote kujenga nyumba ndani ya mita 60, kando na bahari au ziwa, lakini wapo matajiri waliojenga ndani ya maeneo hayo kwa kuvunja sheria, je hawa watu mmewapimia na kuwapa hati?.

Naibu Waziri Mabula.

Jibu:   Sina orodha yao hao unasema wamejenga ndani ya mita 60 nawakapata hati. Aidha wizara inayohusika nmambo ya muungano na mazingira nao pia wanalifanyia kazi jambo hili.

Goryo Swali: Mh waziri kuna hizi nyumba za shirika la nyumba la Taifa NHC zilizo jengwa Mwanza je raia wa kawaida ambaye sii mtumishi anaruhusiwa kukopa nyumba na kama jibu ni ndiyo je anatakiwa awe na vigezo gani?.

Naibu Waziri Mabula.

Jibu:    Nyumba zimejengwa kwa ajili ya Watanzania wote,unaruhusiwa kununua,kukopa au kupanga.Masharti yanatofautiana kutegemea na nini unataka kufanya kati ya hayo niliyotaja hapo juu.

Salome Salehe kutoka mkoa wa Mwanza.

Swali.Mwaka 2010 hapo katika kata ya Igoma, Wilaya ya Nyamagana tulitakiwa kulipa pesa kiasi cha Tzs 150,000/=kwa ajiri ya Upimaji Shirikishi, tulipewa namba za kulipia katika akaunti ya NMB,, baadhi ya wananchi tulilipa kiasi hicho lakini hadi leo hatujapata hatimiliki hiyo, badala yake tumetakiwa tulipe kiasi hicho cha pesa upya eti hizo za awali haijulikani zilienda wapi,je unaweza kunisaidia?.

Naibu Waziri Mabula.

Jibu:   Pole sana hiyo kesi yako ni tofauti cha msingi nikushauri kama mlichanga na hamjapewa basi ni vizuri mkajiorodhesha majina mkapeleka madai yenu kwa kamishna afatilie kujua halmashauri kwanini haijafatilia,nachofahamu kuna upimaji ulikuwa umefanyika awali kabla ya zoezi la urasimishaji,hawawezi kuwapimia tena lazima waangalie  upimaji wa awali labda kama wamejenga kiholela kuna utaratibu wa kubadilisha ramani na watu wakatumia.

Limbe swali:Kuna baadhi ya wananchi wanyonge wa halmashauri ya Chato waliotozwa fedha kiasi cha 30,000 kila kaya kwa lengo la  kupimiwa maeneo yao ili wapate hati za kimila lakini sasa ni zaidi ya miaka miwili hawajawahi kupimiwa,je Serikali inawasaidiaje wananchi hao walioonyesha nia njema ya serikali.

Naibu Waziri Mabula.

Jibu:Sijafahamu kwanini hawajapimiwa labda mpaka kufatilia hilo swala kwasababu maswala ya urasimishaji maeneo mengi walikuwa wanalalamika kutokana na watu waliochanga mwanzo  na sasa kuambiwa kuongeza pesa kutokana na wakandarasi wanaopima labda gharama za upimaji zimeongezeka,swala la msingi tulijue likoje nashauli wapeleke malalamiko kwa Mkurugenzi wa halmashauri ikishindikana wapeleke ofisi zetu za kanda tutawasaidia.

Kaijage, Swali: Kwa uelewa wangu miji  mingi hasa yenye hadhi ya Manispaa katikati ya mji nyumba mbovu inapodondoka au mtu kuuza mnunuzi anapaswa kujenga nyumba angalau yenye hadhi au garofa japo 2 kwa ajiri ya kufanya mji upendeze lakini unakuta watu wanajenga bimu za kuinua ghorofa na wanawaita watu Wa mipango miji wanashauri kisha wanazungushia mabati wakimaliza ujenzi mnakuta imejengwa nyumba ya kawaida sana na zile bimu zimefia hapo,je huoni hii ina sababisha miji kutokuwa ya kisasa na kuwa ya kibiashara.

Naibu Waziri Mabula.

Jibu:Unachokisema ni kweli tatizo linakuwa ni usimamizi hasa Wakurugenzi kwa sababau maeneo yoye hayo kama mtu ana hati yake ya zaidi ya miaka 30 inapokwisha muda wake haruhusiwi tena kujenga tofauti na mpango mji.

Unavyosema inatakiwa kama ni ghorofa ajenge, au nyumba ya kawaida na swala hilo tulishawaambia wahusika ni swala tu la usimamizi ni tatizo tu la watumishi wetu siyo waaminifu wanachukua rushwa matokeo yake wanapitisha vibari vya ujenzi kinyume na mipango miji na sasa hivi wamerudishwa wizara ya ardhi tutawafatilia na watafata taratibu.

Goryo,Swali: Kuna migogoro mikubwa kati ya wanainchi wanaoishi kando kando mwa mbuga za wanyama hususani wilaya ya Tarime kijiji cha Kegonga Mimi ni mzaliwa wa kegonga nimezaliwa nimekuta tunaishi hapo tangu nikiwa mdogo hadi sasa hivi ni mzee na watu wa Tanapa walitujengea kisima hapo cha kuchota maji mwaka 2002 .

Ajabu juzi juzi tumeambiwa tuhame eti tumevamia hifadhi ya Serengeti swali langu kama vijiji viliwakuta wazazi wetu wanaishi hapo na tangu bibi na babu wamezikwa hapo inakuwaje Leo tunapewa notice eti tuhame kutoka maeneo yetu na watu sehemu nyingine ya kwenda kuishi?

Naibu Waziri Mabula.

Jibu: Kwa sasa tunao mradi mkubwa wa miaka 4 ambapo kazi inayofanyika sasa ni kupima maeneo yote yanayopakana na mbuga za wanyama kwenye hifadhi ili kuweka mapango wa matumizi bora ya ardhi na kuondoa migogoro tuna vijiji 392 na mkoa wa Mara tayali tumeshaanza kwa baadhi ya maeneo,nikuombe uwe na subira najua migogoro iko mingi swala hili linashughulikiwa na litaisha naomba mtupe muda kama Serikali kama Wizara tunalifanyia kazi tumeshaona hitaji la wananchi ni kuwapimia maeneo na kuondoa migogoro.

Julius Chacha kutoka Mara.

Swali.Migogoro ya ardhi na vyombo vya ulinzi imekuwa ni tatizo ikiwemo wilaya ya Tarime tathimini zimefanyika lakini hadi sasa watu hawajalipwa,Je Serikali inatoa tamko gani kuhusu ucheleweshwaji wa fidia?.

Naibu Waziri Mabula.

Jibu:Maswala ya fidia yapo katika maeneo mengi nchini lakini nataka kukuthibitishia ni kwamba Jeshi la Ulinzi walishapita kuhakiki mipaka ya maeneo yao na uthamini ulishafanyika na bajeti ya mwaka jana waliweka pesa zaidi ya Bilioni 4 kinachosubiliwa wakipata fedha watalipa fidia nakuomba uwe mvumilivu ikizingatiwa jeshi tunawahitaji kwa ulinzi tuwe wavumilivu mwisho wa yote haki yako utapata.

Kaijage, Swali: Kuna hatua gani zinapaswa kuchukuliwa kwa wenye nyumba wanaopangisha uchocholo kwa wafanyabiashara hawa machinga?yaani uchocholo unaotenganisha nyumba na nyumba.

Naibu Waziri Mabula.

Jibu:Swala lako ni la Halmashauri ni usimamizi tu wamipango miji wanapaswa kuangalia wapi pakuweka biashara na makazi wanapopangisha uchocholoni ni ukiukwaji wa maadili,kinachokatiwa ni usimamaizi wa sheria na wengi wamejisahau mwarobaini wao umekaribia hapa ni kazi tuu hakuna longolongo.

Tuma.Swali:  Mhe. Waziri lipo tatizo la baadhi ya wapangaji wa nyumba za Serikali anapoamua kuhama yeye anayehama anapangisha kwa gharama nyingine kubwa. Naomba kujua, huu ndiyo utaratibu wa Serikali?

Naibu Waziri Mabula.

Jibu:Ungenipa mfano wa watu waliohama  na wakapangisha kwa gharama kubwa nachofahamu hizi nyumba Shirika la nyumba ufanya msako kuwasaka na kuwaondoa.

Kaijage,Swali:Mara nyingi watu Wa Aridhi wakiwa wanapima maeneo wakikukuta unayo maeneo mengi wanataka uwapatie wao viwanja viwili mpaka vitatu je hivi viwanja  huwa ni vya serikali au uchukua wao kama wao?

Naibu Waziri Mabula.

Jibu:Huo ni wizi na taratibu hairuhusiwi na kwa taarifa yako sasa hivi tuna ruhusu kumilikisha mtu maeneo yake yote ilimradi alipe gharama zote ndani ya muda akishindwa maeneo wanagawiwa wengine na yeye anapewa fidia.

Tuma,Swali:Waziri, Pale Somanda Wilaya ya Bariadi kuna mtu alikuwa na eneo lake lenye nyaraka alizopewa na Serikali kumiliki eneo husika, lakini kadhulumiwa na mtu mwenye misuri ya fedha kisha na tajiri huyu amepewa offer ya eneo hilo, amejenga na kuikodishia taasisi ya kiserikali inayosimamia haki za raia. Je, wizara yako inaufahamu huu mgogoro? Na kama inaofahamu, nini tegemeo?.

Naibu Waziri Mabula.

Jibu:Kesi hiyo ifikishwe kwa kamishina ili apitie suala hilo nakulipatia ufumbuzi ikishindikana waende baraza la ardhi la nyumba wilaya.

Shukrani za Wajumbe.

Goryo :Ahsante Naibu Waziri kujitokeza kwenye mjadala umejibu maswali mazuri,majibu yako yanaonyesha ukomavu Mungu akubariki sana.

Jasamila Maduhu kutoka mkoani Shinyanga:Hongera Naibu Waziri kiongozi anayejua  Wizara yake utamjua kwa majibu yake nikuombe tu Wizara yako iendeleee kutoa vipindi mbalimbali vya maswala ya ardhi ikiwemo namna ya uendeshaji wa mashauri ya ardhi .

Josephat Manyenye kutoka Mkoani Geita:Naibu Waziri hongera sana kwa kutenga muda wako pia Mungu akubariki na akutie nguvu ili uendelee kulitumikia Taifa katika uadilifu.

Mkuu wa Kundi la Tanzania yetu Sitta Tuma anahitimisha mjadala huo uliohusu zoezi la upimaji shirikishi ulioilenga Wizara ya ardhi,Nyumba  na Maendeleo ya Mkazi, na niaba  ya wajumbe wa Tanzania Yetu amempongeza Naibu Waziri kwa kushiriki kujibu maswali.

Naibu Waziri Mabula washukuru wana Tanzania Yetu.

Shukrani: Nawashukuru wajumbe wa Tanzania yetu kwa maswali yenu na nalipongeza Kundi hilo kwa kuwa na miadala mbalimbali yakimaendeleo ni vyema  makundi mengine yakaiga nakuwa na mijadala ya hoja za kujenga yangekuwa na umaana kuliko kujikita kwenye mambo yasiyo ya msingi.

Nimpongeze aliyeleta wazo hili,naomba kwa wale Mawaziri wakuu wa mikoa watendaji wa taasisi mbalimbali waliomo kwenye kundi hili basi mara mojamoja mnawaita mnawauliza maswali wanatoa elimu ya kutosha kwa wananchi wetu lakini pia tunapokea ushauri kutoka kwa wadau mbalimbali siyo kwamba ukiwa Waziri au mkuu wa mkoa unajua mambo yote ushauri kutoka kwa wananchi wetu unaweza kuboresha utendaji wetu wa kazi.

Hata hivyo mbali na mjadala huo Tanzania Yetu imekuwa ikitoa mijadala mbalimbali na kujibiwa na Viongezi wa Serikali wakiwemo Manaibu Waziri,waliowahi kujibu maswali ya wajumbe katika mjadala ni Naibu Waziri Kilimo Omari Mgumba .

Waziri Mgumba akishirikiana na Mkurugenzi mkuu Bodi ya Pamba nchini Marco Mtunga walijibu maswali katika mada iliyohoji nini kifanyike  kuokoa mazao dhidi ya wadudu waharibifu na je wakulima wana elimu ya kutosha namna ya kujikinga na madhara ya dawa za kuuwa wadudu ambazo zina kemikali?.

Wengine ni Naibu Waziri wa afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Faustine Ndugulile ambaye alijibu maswali kuhusiana na mada iliyohusu nini kifanyike kukomesha ukatili wa kijinsia ,mimba na Ndoa za utotoni, Afisa habari kutoka  mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)Rose Mdami alijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa kuhusu Vitambulisho vya Taifa.

Katika Wizara ya Uvuvi na Mifugo ilijadiliwa mada iliyohusu uvuvi haramu na uvuvi unaozingatia sheria,una madhara na faida gani kiuchumi? ambapo Naibu Waziri wa uvuvi Luhaga Mpina aliahidi kujibu maswali ya wajumbe lakini hata hivyo hadi muda wa mjadala huo unamalizika hakujitokeza kujibu chochote wala kueleza sababu za kutoshiriki kwenye mjadala licha yakuandaliwa na kuahidi kushiriki jambo ambalo liliwasikitisha na kuwakwanza baadhi ya wajumbe

 

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.