RUSSIA:HATUKOSI USINGIZI HATA KIDOGO KWA VITISHO VYA MAREKANI

Moscow, RUSSIA.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergey Ryabkov, ametangaza kuwa nchi yake haishughulishwi na matamko na amri iliyotangazwa na Marekani kutekeleza vitisho vyake kuhusu kujitoa katika Mkataba wa Silaha za Masafa ya Wastani za Nyuklia (ANF).

Waziri Ryabkov amenukuliwa na shirika la habari la RIA Novosti akisema hayo na kuongeza kuwa mkataba wa ANF uko wazi na umekuwa ukitangazwa waziwazi hadharani, hivyo, vitisho na amri zinazotolewa na Marekani kuhusu mkataba huo hazikubaliki kabisa.

Marekani inaituhumu Russia kuwa inakanyaga vipengele vya mkataba wa ANF, hivyo Marekani imeamua kusimamisha utekelezaji wake na imetishia kuwa kama Russia haitatoa ahadi za vitendo basi itajitoa kabisa katika mkataba huo.

Russia imekanusha madai hayo na kusema haishughulishwi na vitisho hivyo vya Marekani.

Ryabkov pia amelalamikia ujumbe wa Marekani kuhusu mazungumzo ya Trump na Putin na kusema kuwa, Russia haikubaliani na madai yanayotolewa na Marekani juu ya uamuzi wa Trump wa kuvunja mazungumzo yaliyokuwa yameshapangwa tangu huko nyuma kwa kisingizio cha mgogoro wa Ukraine.

Amesema mazungumzo hayo yaliyopangwa kufanyika mwakani ni muhimu kwa pande zote mbili, hivyo Marekani ina wajibu wa kuheshimu ahadi zake na kuachana na michezo yake ya kurubuni hisia za wengine.

Aidha, kiongozi huyo ameongeza kuwa Taifa hilo kubwa (Marekani) linapaswa kubeba lawama, kutokana kuchochea mahusianao mabaya baina yake na Russia, na kusisitiza kuwa wao hawataibembeleza Marekani kwa mazungumzo hayo maana ndio wanaohusika na hali (mbaya) iliyopo hivi sasa.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.