MANARA ATANGAZA MWAKA WA KUACHA KAZI SIMBA SC

Na Shabani Rapwi.

Afisa Habari wa klabu ya Simba SC, Haji Manara ametangaza kuachana na klabu hiyo, baada ya kuwepo kwa tetesi ya kutemwa katika nafasi hiyo.

Leo February 10, 2019 kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara amesema kuwa anafahamu kuwa mashabiki wengi wa Yanga hawapendi kumwona akiwepo Simba na siku atakayoondoka watafanya sherehe.

“Kuna watu wa Yanga hamu yao nife kabisa, nawaumiza sana na siku mtakaposikia sipo kikazi Simba, mtafanya sherehe. Ila nikuhakikishie kuwa Mungu akinipa uhai nitaacha kazi Januari 2021 tena kwa hiari” alisema Manara.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.