MAKONDA AWAPA MIKAKATI YA KUKUSANYA MAPATO WAKURUGENZI.

 

Na, HERI SHAABAN.

MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameeleza Mikakati ya ukusanyaji Mapato kwa Wakurugenzi wa Mkoa huo.

Agizo hilo Makonda alilitoa Dar es Salam leo wakati wa kikao cha Mkakati wa Mpango wa ukusanyaji mapato baina yake na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wote wa Mkoa Dar es Salam.

Aliwataka Wakurugenzi kubuni mbinu za ukusanyaji wa vyanzo vya mapato ili kuongeza idadi ya walipa kodi ambapo alisema kwa Mwaka huu jiji hilo limedhamiria kuongeza wigo wa ukusanyaji mapato na kuendelea kuwa kinala.

“Vyanzo vipo vingi vya Mapato nakuagiza Mkurugenzi wa Ilala Jumanne Shauri, naomba uzungumze na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege pale nyuma ya jengo lao kijengwe kituo cha daladala kipya Banana ili magari yote yashushe abiria ndani mtapata mapato ya kutosha na pale nje itasaidia kuondoa msongamano wa magari kwani yote yatamia kituoni ” alisema Makonda.

Makonda aliwataka kufanya mabadiliko ya sheria kandamizi zilizopitwa na wakati pamoja na kuanzisha mfumo wa malipo kwa kadi kama ilivyo mataifa mengine.

Aidha alimwagiza Mkurugenzi wa KINONDONI kujenga kituo cha daladala eneo la Kawe Kwa ajili ya kuondoa msongamano wa magari.

Pia aliagiza kuanzishwa kitengo cha ushauri Kwa Wafanyabiashara Jambo litakalo wajengea Wananchi hamasa ya kulipa kodi
na kuondoa dhana ya kuonekana watu wa kukusanya mapato pekee.

Alisema ana imani Wananchi wa Mkoa huo Wapo tayari kulipa kodi endapo Serikali watawezesha kulipia ikiwa ni pamoja Wafanyabiashara kuwaweka katika mfumo maalum wa kuifadhi kumbukumbu.

Makonda alisema mkutano huo umewashirikisha pia na TRA, BOT, TIC, NBS,Wizara ya FEDHA na Kamati za Ulinzi na Usalama mkoa Dar es Salam.

Aliziagiza Halmashauri zote zilizopo mkoa huo kuwachukulia hatua Wafanyabiashara wote wakwepaji Wa kulipa kodi na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Wakati huohuo MAKONDA aliwagiza Wakuu wa Wilaya zote kuwatambua Wafanyabiashara Machinga kama Wafanyabiashara wa kati wapewe kipaumbele.

“Mh. Rais amewatambua Wafanyabiashara wote na ametoa vitamburisho Kwa gharama za shilingi 20,000 hivyo tuwatambue rasmi na kuunga mkono juhudi zake na Serikali ya awamu ya tano ya kukuza uchumi wa Viwanda “alisema Makonda.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.