MAKONDA ASAINI MIKATABA YA LISHE NA WAKUU WA WILAYA ZA DAR

Na Heri Shaaban

Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewataka wakuu wa Wilaya zote kuakikisha Manispaa zao zinafanya vizuri katika kuzingatia suala la lishe, na wanapoingia katika vikao vyao vya baraza la Madiwani suala hilo iwe sehemu ya ajenda kila siku.

Akizungumza mkoani humo, jana na wakuu hao mara baada ya kutiliana saini hiyo, ambapo amesema katika wilaya zote tano, Temeke Iĺala na Kinondoni ndio zina idadi kubwa ya watoto hivyo, ni vyema wakaenda kutoa elimu ya lishe pamoja na kujikinga na Utapia mlo ili waweze kukabiliana na changamoto hiyo.

Aidha amezitaka kamati za Afya wilaya zote kuzingatia usafi pamoja na makatibu Tawala na wakuu wa wilaya pamoja na wananchi kwa ujumla, huku akiwataka wanawake wajawazito kuzingatia lishe katika siku 1000 za ujauzito na miaka miwili ya ukuaji mtoto.

Kwa upande wake Ofisa Lishe Mkoa wa Dar es Salaam,Janeth Mzava amesema mkoa huo, una mikakati saba ya kutoa elimu ya lishe ngazi ya jamii pamoja na kuongeza virutubisho katika vyakula.

Amesema kuwa, vyanzo vya fedha katika utekelezaji wa shuguli za lishe zinatokana na wadau na serikali, kupitia mapato ya ndani (OS) mapato ya matumizi mengine (OC) na mfuko wa pamoja wa afya (HSBF)kupitia vyanzo vya Serekali.

Aidha, ameitaja Halmashauri iliyofanya vizuri katika mikakati ya lishe, kuwa ni wilaya Temeke kwa kutoa fedha zilizotengwa, ilala ikiwa ya pili wilaya inaonyesha kutumia shilingi milioni 100 ĺakini wanaonekana wametumia milioni 44, na Kigamboni milioni 27 lakini wametumia 2,460,000.

Naye, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Grace Magembe, amesema, kazi iliyobaki kwa wakuu wa wilaya wote kwenda kusaini mkataba wa lishe kwa Mkurugenzi wa manispaa pamoja na Mchumi awepo.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.