MAHAKAMA YAAMURU MWILI WA MAREHEMU UFUKULIWE ILI UCHUNGUZWE

Na Stephen Noel Mpwapwa .


Mahakama ya Hakimu mkazi wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma imeamuru kufukufukuliwa kwa mwili wa marehemu Cosmas Msote aliye fariki miezi mitano ili ufanyiwe uchunguzi wa chanzo cha kifo chake.

Mahakama hiyo imefikia uamuzi huo baada ya kuwapo na ubishani Kati ya taarifa zilizo andikwa na Mganga wa hospital ya wilaya ya Mpwapwa juu chanzo cha kifo cha bwana Cosmas Msote aliye fariki dunia tarehe 5 October 2018.

Kwa mujibu wa Hakimu mkazi wa Mahakama ya wilaya ya Mpwapwa bwana Pascal Mayumba amesema aliamua kutoa kibali hicho kutokana na kuwapo sintofahamu ya chanzo kifo cha marehemu huyo.

Aidha hakimu Mayumba ameiambia mahakama Polis wilayani hapa waliomba ombi la kufukua mwili wa marehemu Cosmas Msote baada ya kuwapo kwa malalamiko ya kuwa kifo chake kilitokana na kipigo na si shinikizo la damu kama inavyo daiwa.

Ofisa upelelezi wa polis mjini Mpwapwa bwana Makubura Kati amesema ndungu wa marehemu walileta lalamiko kuwa kifo cha ndugu yao kilitokana kipigo na alizikwa kabla mwili wake hujafanyiwa uchunguzi yaani (postmotum).

Na alisema kutokana na malalamiko hayo wanamshikilia kijana mmoja aliye fahamika kwa jina la Emanuel Sindato kwa tuhuma za marehemu huyo.

Mmoja wa watoto wa marehemu bwana Julias Msote amesema kuwa wameamua kufukua mwili wa baba yao baada ya kubaini kuwa kifo chake hakikutokana na shinikizo la damu kitu alicho kisema kipigo.
Hata hivyo bwana Julias amesema kuwa mwili wa baba toka wanaufikisha hospitalin walisema ulitokana na kipigo na Fomu ya polis namba tatu walijaza (PF3)sasa ninashangazwa kuambiwa mzee Alifariki kwa presha tatizo ambalo hajawahi kuwa nalo Katika maisha yake yote,”aliongea Julias

Aidha amesema wanasubiri taarifa ya daktari alifanya uchunguzi huo na kubain chanzo cha kifo cha marehemu.

Uchunguzi huo ulifanywa na mganga mkuu mfawidhi wa hospital ya wilaya Dkt Hamza Mkingule na bibi Afya wa wilaya bi Merry Mabagwa chini ya uangalizi wa polisi wa kituo kikuu cha wilaya.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.