MAHAKAMA KUU KIGALI YAMUACHIA HURU RWIGARA NA MAMA YAKE..

Mahakama Kuu mjini Kigali imemuachia huru kwa dhamana mwanasiasa wa upinzani Diane Rwigara na mamake Bi.Adeline Mukangemanyi Rwigara ambaye ameshtakiwa kwa makosa ya kuchochea uasi.

Jaji wa mahakama kuu mjini Kigali ametangaza kwamba maombi yao ya dhamana yamekubaliwa lakini wamewekewa masharti ya kukabidhi pasipoti zao kwa mwendesha mashitaka, na pia wametakiwa kutovuka mipaka ya jiji la Kigali bila kuwa na kibali maalumu.

Chanzo Cha habari kinasema baada ya uwamuzi huo umati wa jamaa zao uliimba na kusherehekea mahakamani hupo wakimsifu Mwenyezi Mungu kwa uamuzi huo uliotolewa.

Wawili hao walikuwa kizuizini tangu mwaka jana kwa tuhuma za kuchochea vurugu na mgawanyiko miongoni mwa wananchi pamoja na kughushi nyaraka.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.